Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, akiongoza kikao cha Maafisa Masuhuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua (katikati), akisisitiza umuhimu wa Wizara, Taasisi na Mashirika ya Umma yanayokusanya mapato yasiyo ya kodi kutumia kikamilifu fursa zilizopo ili kuongeza mapato ya ndani wakati wa kikao na Maafisa Masuhuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square. Kushoto ni Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie na kulia ni Kamisha Msaidizi Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha Bw. William Mhoja.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Agnes Meena na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo Bi. Eleonora Saitoria wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.

Kamisha Msaidizi Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha Bw. William Mhoja akiwasilisha maelezo kuhusu mwenendo wa ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi wakati wa kikao cha Maafisa Masuhuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.

Manaibu Kamishna wa Idara ya uchambuzi wa Sera Wizara ya Fedha Bw. Juma Mkabakuli (Kushoto) na Dkt. Iddy Kayumba wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.

Mchumi, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha Bi. Jenipher Rauya akitoa wasilisho kuhusu mwenendo wa mapato yasiyo ya kodi, wakati wa wakati wa kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.

Afisa Usimamizi wa Fedha Mkuu, Idara ya Uchambuzi wa Sera Bi. Emerensiana Nyanda, akifanya wasilisho kuhusu mrejesho wa utekelezaji wa maazimio yatokanayo na kikao cha Maafisa Masuuli kilichofanyika Septemba 2025/206, wakati wa kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Masuuli, wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, baada ya kumalizikia kwa kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Masuuli, wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, na baadhi ya wajumbe wa kikao baaada ya kumalizikia kwa kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Tehama, Wizara ya Fedha, Dkt. John Sausi, akifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Kikao cha Maafisa Masuuli, wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi baaada ya kumalizikia kwa kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
Na. Josephine Majura na Abdul Madenge, WF, Dodoma
SERIKALI imezitaka Wizara, Taasisi na Mashirika ya Umma yanazokusanya mapato yasiyo ya kodi kutumia kikamilifu fursa zilizopo ili kuongeza mapato ya ndani na kuimarisha uwezo wa Serikali kugharamia huduma za wananchi na miradi ya maendeleo.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, katika kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika katika Ofisi za Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma.
Bw. Joshua amesema bado kuna fursa nyingi za mapato ambazo hazijatumika kikamilifu, huku takwimu za mwaka wa fedha 2025/26 zikionesha kuwa mafungu Matano kati ya 26 yanayokusanya mapato yasiyo ya kodi ndiyo yaliyofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato.
“Ni muhimu kila fungu kujitathmini, kubaini changamoto zinazokwamisha ukusanyaji na kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha malengo yanafikiwa,” amesema Bw. Joshua.
Hata hivyo, amesema makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi yameonesha ukuaji, ambapo katika kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka wa fedha 2026/27, ambapo Serikali ilikusanya zaidi ya shilingi trilioni moja, sawa na asilimia 114.1 ya lengo na ongezeko la asilimia 32.7 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2025.
“Taasisi zenye ufanisi wa chini ya asilimia 50 zinapaswa kubaini changamoto mahsusi na kuweka mikakati ya kuzitatua ili kuboresha ukusanyaji na kufikia malengo ya mwaka wa fedha 2026/27,” amesisitiza Bw. Joshua
Ameeleza kuwa kuimarisha mapato ya ndani ni muhimu kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya Serikali, ikiwemo kugharamia miundombinu na huduma za kijamii ambapo katika kipindi cha miaka mitano, bajeti ya Serikali imeongezeka kwa asilimia 50.3, kutoka shilingi trilioni 41.5 mwaka 2022/23 hadi shilingi trilioni 62.3 mwaka 2026/27.
Bw. Joshua amezitaka taasisi husika kutekeleza maazimio ya kikao kazi cha wataalamu kilichofanyika Oktoba 21 hadi 22, 2026, huku akisisitiza kuwa Wizara ya Fedha itaendelea kutoa ushirikiano kutatua changamoto za kimfumo na kiutendaji ili kuhakikisha kila fungu linafikia malengo yake ya ukusanyaji wa mapato.
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi, Kamisha Msaidizi Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha Bw. William Mhoja, amesema kikao hicho ni muhimu katika kutathmini utekelezaji wa malengo ya ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 na kuweka mikakati madhubuti, shirikishi na inayopimika kwa mwaka 2026/2.
Ameeleza kuwa kikao cha mwaka huu cha Maafisa Masuuli wanaokusanya mapato yasiyo ya kodi kilitanguliwa na kikao cha wataalamu kwa lengo la kubaini changamoto na kuandaa mikakati itakayowezesha Wizara, Taasisi na Mashirika ya Umma kuongeza ufanisi wa ukusanyaji na kuhakikisha Serikali inafikia malengo yake ya mapato.
Mapato yasiyo ya kodi ni fedha zinazokusanywa na Serikali kupitia huduma na shughuli za taasisi zake ambapo mapato hayo huongeza uwezo wa Serikali kugharamia huduma muhimu kwa wananchi, ikiwemo afya, elimu, maji na Barabara, hivyo ufanisi wake husaidia kuhakikisha Serikali inapata fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo na kuboresha mais ha ya wananchi.