Featured Michezo

YANGA BINGWA ASFC 2021/22,YAICHAPA COASTAL UNION KWA MATUTA

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin-ARUSHA

KLABU ya soka ya Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa  Kombe la Shirikisho maarufu ‘Azam Sports Federation Cup’ (ASFC) baada ya kuichapa Coastal Union  mabao 4-1 kwa  mikwaju ya penati mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Abeid Karume jijini Arusha.

Mchezo ulilazimika kwenda hatua ya mikwaju ya penati ikiwa ni baada ya timu zote mbili kulazimishana sare ya mabao 3-3 katika kipindi cha dakika 120.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Feisal Salum, Herittier Makambo Pamoja na Denis Nkane huku yale ya Coastal Union yakifungwa na Abdul Suleiman Sopu aliyefunga mabao yote matatu Hat Trick.

Kwa ushindi huo Yanga imeendelea kutopoteza mchezo wowote katika mashindano yote ya ndani kwa maana ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya NBC Pamoja na Kombe la Shirikisho.

Wachezaji wa Yanga waliopata mikwaju ya penati ni Yannick Bangala, Dickson Job, Herittier Makambo Pamoja na Khalid Aucho huku ile ya Coastal Union likifungwa na Victor Akpan.

Kwa sasa Tanzania itawakilishwa na Yanga SC pamoja na watani zao wa jadi Simba SC kwenye klabu bingwa Afrika (Caf Champion League) huku Azam FC na Geita Gold FC zitashiriki kombe la shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup).

About the author

mzalendoeditor