Featured Kitaifa

ZIMAMOTO YAPOKEA UGENI TOKA JIJI LA HAMBURG

Written by mzalendoeditor

Kaimu Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, DCF Charo Mangare akisoma taarifa yake, kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mara baada ya kupokea ugeni kutoka Jiji la hamburg nchini Ujerumani, katika Maadhimisho ya sherehe ya miaka 12 ya ushirikiano kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg, hafla iliyofanyika leo Julai 2, 2022 katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Mazingira Jimbo la Hamburg, Michael Pollmann akilishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kusimamia vema vitendea kazi na mafunzo wanayowapatia kwa kipindi cha miaka 12 ya mashirikiano kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg, hafla iliyofanyika leo Julai 2, 2022 katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam.

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitengo cha Maokozi wakionesha umahiri wao mbele ya ugeni toka Jiji la Hamburg jinsi ya kufanya uokoaji kwenye majengo marefu pindi madhara yanapotokea wakati ugeni huu ulipowasili katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Maafisa, Askari na Wageni mbalimbali walioshiriki katika Maadhimisho ya sherehe ya miaka 12 ya mashirikiano kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg, hafla iliyofanyika leo Julai 2, 2022 katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam.

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Nyanda, akitoa maelezo mbele ya ujumbe toka Jiji la Hamburg, vifaa vya msaada walivyopatiwa na Jiji hilo vinavyolisaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kutekeleza majukumu yake, wakati ugeni huu ulipowasili katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam

Katibu wa Mazingira Jimbo la Hamburg, Michael Pollmann (katikati), Kaimu Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (DCF) Charo Mangare (Wapili kushoto), Mratibu wa Uhusiano kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg Bi.  Inken Bruns (Wapili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Uokoaji Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (DCF) Bashiri Madhehebi (kulia), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo pamoja na ujumbe toka Jiji la Hamburg wakati ugeni huu ulipowasili katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam leo Julai 2, 2022.

 (PICHA NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI)

…………………………………..

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM 

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini limepokea Ugeni toka Jiji la Hamburg ikiwa ni maadhimisho ya miaka 12 kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg. Kwa kipindi cha miaka 12 ya ushirikiano baina ya Jiji la Dar es Salaam na Hamburg nchini Ujerumani, Jeshi hilo limefanikiwa kupata mafunzo ya uzimaji moto, maokozi na vifaa vya uokoaji nchini.

Akisoma taarifa yake kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kaimu Kamishna wa Operesheni DCF Charo Mangare alipokuwa akipokea ugeni huo. Alisema ndani ya miaka hiyo 12 tumeweza kupata mafunzo mbalimbali pamoja na kubadilishana programu kati ya majiji haya mawili. Zaidi ya Maafisa na Askari 48 wamenufaika na programu za maafunzo kutoka jijini Hamburg.

Shukrani za pekee ziende kwa Mratibu wa Uhusiano huu, Bi. Inken Bruns na Mratibu wa Zimamoto, Bw. Reinhard Paulsen.

Upande wake Katibu wa mazingira Jimbo la Hamburg, Michael Pollmann alisema amefurahi kuona mafunzo waliyoyatoa yanafanyiwa kazi iliyokusudiwa kwa vitendo.

Nimeona kupitia mafunzo hayo wameweza kujisimamia na kuyaendeleza kupitia uzoefu walioupata kwa sababu Zimamoto ni eneo nyeti linalookoa Maisha na Mali za watu mijini na vijijini.

About the author

mzalendoeditor