Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kushoto) akiwa katika picha na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF anayesimamia Idara ya Afrika, Bw. Zeine Zeidane, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha SDKJ, Banjul nchini Gambia, pembezoni mwa Mikutano ya African Caucus ya Mwaka 2026, ambapo pamoja na mambo mengine, Ujumbe wa Tanzania na IMF walijadili namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Taasisi hiyo muhimu ya fedha.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF anayesimamia Idara ya Afrika, Bw. Zeine Zeidane (wa tatu kulia), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil (wa pili kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Adran Ubisse, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha SDKJ, Banjul nchini Gambia, pembezoni mwa Mikutano ya African Caucus ya Mwaka 2026, ambapo pamoja na mambo mengine, Ujumbe wa Tanzania na IMF walijadili namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Taasisi hiyo muhimu ya fedha.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF, Banjul, Gambia)
Na Benny Mwaipaja
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kulia), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF anayesimamia Idara ya Afrika, Bw. Zeine Zeidane, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha SDKJ, Banjul nchini Gambia, pembezoni mwa Mikutano ya African Caucus ya Mwaka 2026, ambapo pamoja na mambo mengine, Ujumbe wa Tanzania na IMF walijadili namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Taasisi hiyo muhimu ya fedha.
Bwana Zedaine amechukua nafasi ya mtangulizi wake, Bw. Abebe Selassie, ambaye muda wake wa kushikilia nafasi hiyo ulifikia tamati hivi karibuni.
Tanzania imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) tangu ilipojiunga na IMF tarehe 10 Septemba 1962, ambapo jumla ya ahadi ya mikopo ya IMF kwa Tanzania imefikia SDR bilioni 3.27. Kati ya kiasi hicho, portfolio hai ya sasa ni SDR bilioni 1.8.
Kwa ujumla, ushirikiano wa Tanzania na na IMF umekuwa nguzo muhimu katika kuchochea maendeleo ya taifa, hususan kupitia uwekezaji katika miradi ya maendeleo na msaada wa kifedha, kiufundi na kitaalam.
Kwa upande wa Tanzania, Kikao hicho kilimshirikisha pia Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.