Featured Kitaifa

EALA KWA KUSHIRIKIANA NA IDEA YAWAKUTANISHA WANAWAKE WANASIASA KUTOKA NCHI ZA KANDA MBALIMBALI AFRIKA.

Written by mzalendoeditor
Katibu  wa Umoja wa wabunge wanawake wa Bunge la Afrika mashariki (EALA) Fatuma Ndangiza akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo.
Msemaji wa Wabunge wanawake katika bunge wa la jumuiya ya Africa mshariki Mhe.Pamela Maasai  ambaye ni mbunge kutoka Tanzania akifafanua jambo juu ya mkutano wa viongozi wanawake.
Sifisisami Dube mratibu wa shirika la kimataifa la  IDEA akiongea na waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiza jambo katika mkutano huo.
………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Bunge la juimuiya ya Afrika mashariki(EALA) kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la IDEA wamewakutanisha wanawake wabunge/wanasiasa kutoka nchi mbalimbali za Kanda za Afrika ikiwemo EAC, SADIC, COMESA NA ECOWAS.  
Akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha na Katibu  wa Umoja wa wabunge wanawake wa Bunge la Afrika mashariki EALA Fatuma Ndangiza  ambaye pia ni mbunge kutoka Rwanda alisema mkutano huo wa siku tatu utawakutanisha wanawake ambapo wataweza kujadili changamoto za kiuongozi kwa mwanamke lakini pia na mafanikio.
Alieleza kuwa pamoja na changamoto pia watapeana uzoefu utakaosaidia kuongeza wigo au hamasa kwa wanawake kushiriki katika siasa   ili kufikia malengo ya azimio la Beijing la kufikia walau asilimia 30 ya wanawake viongozi kwa kila nchi  ambapo kwa sasa imefikiwa bado ni chini asilimia 30 
“Ni mkutano mkubwa ambao utajadili masuala ya uongozi kwa wanawake barani Afrika, wanayokutana nayo ili kupata uzoefu utakaosaidia watoto wa kike kufikia malengo yao katika kuomba nafasi mbalimbali za uongozi,”Alisema
Kwa upande wake Msemaji wa Wabunge wanawake katika bunge hilo Mhe.Pamela Maasai amesema kuwa mkutano huo umelenga kuwaleta wabunge wanawake pamoja kutoka maeneo mbalimbali ya Jimuiya za Kikanda kuweka mitazamo ya pamoja itakayoleta matokeo chanya ndani na nje ya Jumuiya.
Kwa Upande wake Sifisisami Dube mratibu wa IDEA ambao ndio wadhamini wa mkutano huo alisema kuwa taasisi hiyo  inafanyakazi chini ya mwamvuli wa ubalozi wa Sweden ambapo wanalenga kazi tatu muhimu ikiwemo kusaidia masuala ya uchaguzi ushiriki wa kisiasa kwa wanawake na kufanya masuala ya katiba katika nchi zinazohitaji kusaidiwa katika masuala hayo.
“Lakini katika mkutano huu tumejikita katika kitu kimoja ambacho ushiriki wa wanawake katika nyanja ya siasa pia tuna kipengele cha vyombo vya habàri vinavyojihusisha katika kusukima ajenda mbalimbali za ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya kisiasa,”Alisema.
Hata hivyo mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na spika wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ambaye pia atashirikisha changamoto na mafanikio aliyoyapata katika suala zima za siasa

About the author

mzalendoeditor