Featured Kitaifa

SPIKA DKT. TULIA AMUONYA MBUNGE MWITA WAITARA

Written by mzalendoeditor

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema kitendo Cha Mbunge Mwita Waitara kupinga na kuhoji uamuzi wa Spika Sio sawa na ni kinyume Cha Maadili ya Kanuni za Bunge
Dkt. Tulia amesema Waitara ametoa malalamiko hayo kupitia gazeti la Raia Mwema

Spika amesema jambo hilo alishalitolea uamuzi lakini Mbunge huyo alilalamika kinyume na kanuni na taratibu za kibunge kwa kulalamika Kwenye vyombo vya Habari

Kwa Mujibu wa Sheria za Bunge zinazuia Mbunge kuvunja heshima kwa Spika na inaruhusu kutoa adhabu kwa kushusha hadhi kwa Spika.

Amesema kwa kutumia Mamlaka ya kusimamia matumizi sahihi ya Kanuni za Bunge hivyo kutokana na kitendo Cha utovu wa nidhamu Cha Mbunge huyo amepewa onyo la kutokurudia kudharau maamuzi ya Spika.
“Nampa onyo asirudie kufanya kosa hilo, na baada ya kumpa onyo hilo namsamehe”Spika Dkt.Tulia

Mnamo Tarehe 09 Juni Spika DKT. Tulia alitoa Taarifa juu ya Ushahidi wa Wabunge wawili Mhe. Philip Mulugo na Mwita Waitara ambapo alisema wamewasilisha malalamiko kuhusu Watu kuuwawa na siyo ushahidi na hivyo Spika alitoa maagizo kwa Serikali ndani ya Miezi mitatu kuleta Taarifa ya Uchunguzi.

About the author

mzalendoeditor