Featured Kitaifa

UPO ULAZIMA WA KUWAANDAA WATAALAMU TOKA SHULENI.

Written by mzalendoeditor
Mhadhiri msaidizi wa chuo Cha ufundi Arusha (ATC) ambaye pia ni mratibu wa mradi huo Busumabu  Jacob ,akiongea na waandishi wa habari.
Meneja wa mradi wa taasisi ya  Future STEM Business Leaders Josephine Sepeku akiongea na waandishi wa habari juu ya mradi huo.
 kaimu Mkurugenzi mtendaji wa atamizi ya DTBi- COSTECH Dkt Erasto Mlyuka
akifungua mafunzo ya wanafunzi wa kidato Cha sita na tano mkoani Arusha.
………………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Imeelezwa ili kuwa taifa likue katika nyanja za sayansi na teknolojia upo ulazima wa kuwaandaa wataalamu kwanzia shuleni  jambo litakalosaidia kupata watafiti na wabunifu watakabuni  mambo yatakayoleta suluhu ya masuala mbalimbali katika jamii.
Hayo yalisemwa na Dkt Erasto Mlyuka kaimu Mkurugenzi mtendaji wa atamizi ya DTBi- COSTECH wakati akifungua mafunzo yaliyotolewa kwa wanafunzi wa kidato cha tano  na sita na taasisi ya  Future STEM Business Leaders kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)  ambapo alisema kuwa ustawi wa uchumi wa nchi utegemea wataalamu wa ndani  hivyo kupitia program hiyo ya sayansi teknolojia na ubunifu itasaidia kuweza kuwapata wataalamu watakaokudhi katika kutatua changamoto zinazohitaji majawabu katika jamii 
“Mradi huu ulianzia kwenye vituo vya kitaaluma ili kukuza mawazo na kuyapeleka katika ubunifu na pia kuyabadilisha na kuwa bidhaa na kisha kuyapeleka sokoni na kutumika kwenye jamii, tulianza na shule 5 kwa mwaka 2019 na tulikuwa na wanafunzi 40 Mpaka sasa tunao wanafunzi 85 na shule 17 pia tulianzia Dar-es-salaam lakini sasa tupo Arusha,”Alisema  Dk Mlyuka.
Alifafanua kuwa mtu anapokuwa na wazo ni lazima awe na mbunifu kwa kile anacho kiona kwenye jamii ili kuweza kupata suluhisho ya jambo hilo, Ili kufanya wazo hilo liwe na manufaa kwa jamii ambapo pia wazo hilo linatakiwa liwe  na ubora wa kutoa matokeo chanya pale itakapotumika na jamii ikiwemo  kutoa ajira hivyo ni vema mtu akiwa na wazo awe na upeo mkubwa wa kufikiria na aweze kulifanyia kazi kwa haraka.
Aidha aliwataka wanafunzi kuwa wepesi katika kuomba ushirikiano kwa walimu wao pamoja na wataalamu ili kufanikisha ubunifu walioubuni  na kupata matokeo chanya kama   taasisi ya Phizikia ya uingereza walivyofanya na wao wanaweza kufanya zaidi kwani  wakifanya kwa ubora wataweza kufanya bunifu zao kuwa bidhaa kwa haraka na kuingia sokoni na kuleta  suluhisho.
Alisema Wizara ya Elimu sayansi na teknolojia kwa kushirikiana na tume ya sayansi na teknolojia pamoja na taasisi zote zinahusika na maswala ya sayansi na teknolojia kwa kupitia sehemu hizo zote zitahakikisha ubunifu wao unafika sokoni ndiyo maana ni lazima kushirikiana na wataalam mbali mbali pamoja na taasisi hizo za sayansi na teknolojia.
Kwa upande wake Meneja wa mradi huo Josephine Sepeku alisema kuwa madhumuni ya mradi huo ambao ni maalum  wanafunzi wa kidato cha tano na sita ni kusaidia sayansi ubunifu na biashara kwa kukuza mawazo  waliyonayo kuwa halisi na kuleta majawabu katika jamii .
“Tunapo sema Tanzania ya viwanda ili kuwe na viwanda lazima tuwe na wataalamu wa kutosha na ndiyo maana tunaanza kwa kutoa mafunzo ya nadharia ili kuzidi kuwajengea uwezo wanafunzi kwanzia wakiwa shuleni na baada ya mafunzo haya  shule zote shiriki zitashindwanishwa na washindi watapata mafunzo zaidi ya wiki sita ili kuzidi kuwaboresha zaidi katika ubunifu,” Alisema Sepeku.
Alisema kuwa Sepeku tangu kuanzishwa kwa  mradi huo wameshaanza kufanya tafiti mbali mbali ambazo zitawasaidia na wamepanga kutoa mapendekezo katika mitaala ya elimu na wamelenga sayansi ya biashara ni kuweza kuwaondolea wanafunzi msongamano wa utafutaji wa ajira na badala yake wataweza kujiajiri.
Naye Busumabu  Jacob mhadhari msaidizi wa chuo Cha ufundi Arusha  ambaye pia ni mratibu wa mradi huo alisema kuwa wanafunzi hao kwa siku nne watafundishwa namna ya kutatua matatizo katika jamii na baada ya hapo kila shule itakuwa na business menta ambaye ataenda kuibua bunifu zao  na kunganisha na biashara.
“Shule hizi pia zitapata nafasi nyingine ya kuja hapa chuoni kwaajili ya kuja kuonyesha bunifu zao walizoziibua ndani ya miezi sita ijayo ambapo  watakuwa na nafasi ya kushindanishwa na washindi watano watapewa internship kwa kuunganisha na taasisi au kampuni zinazoendana na bunifu walizofanya ili kuweza kubobea zaidi,” Alieleza.
Nao baadhi ya wanafunzi Miracle Innocent kutoka shule ya St Merys Duluti na Stanley Stanley  kutoka shule ya Edmondrise walisema kuwa kuna matatizo mengi katika jamii hivyo elimu wanayoipata juu ya bunifu za kisayansi na kuweza kuzibadilisha kuwa biashara itasaidia kubadilisha jamii lakini kufanya changamoto hizo kuwa fursa kwa kutengeneza ajira lakini pia kutafuta njia rahisi kwa kila mwananchi kuweza kumudu gharama zinazotakiwa katika suluhu watakazozipeleka katika jamii.

About the author

mzalendoeditor