Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Clara Kalanga Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 115 ya Siku ya Wanawake Duniani.
Kalanga alieleza kuwa pamoja na jitihada hizo, bado kuna changamoto kubwa za pengo la kijinsia duniani, akitaja takwimu za UN Women zinazoonesha wanawake wanalipwa ujira mdogo kwa takribani asilimia 23 ikilinganishwa na wanaume, huku zaidi ya wanawake bilioni 2.7 wakikosa uhuru wa kuchagua kazi sawa na wanaume katika baadhi ya maeneo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Clara Kalanga Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 115 ya Siku ya Wanawake Duniani.
Awali akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Dada Gemma Akilimali, alisema maadhimisho ya mwaka huu ni zaidi ya sherehe bali ni wito wa kuchukua hatua za kuvunja mifumo kandamizi na sheria za kibaguzi zinazozuia wanawake na wasichana kupata haki sawa katika jamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Dada Gemma Akilimali.
Alisema kuwekeza kwa wanawake ni mkakati muhimu wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, akisisitiza kuwa mwanamke akipewa nafasi na kuwezeshwa, jamii nzima hunufaika na maendeleo endelevu.
Washiriki mbalimbali wakiendelea kusikiliza katika maadhimisho ya miaka 115 ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Mabibo Dar es salaam.
Munaa Theatre arts Group wakitoa burudani kwa njia ya Maigizo kwa lengo la kuelimisha juu ukatili wa Kijinsia
Alex Shayo Mratibu wa Mtakuwawa ii, kutoka wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia wanawake na Makundi maalum, akitoa mada katika maadhimisho hayo.
Happiness Maruchu Mwanaharakati WA Masuala ya Bajeti.
Cajentan Tumaini mwansheria kutoka Dawati la Familia, kutoka kituo Cha Sheria na Haki za binadamu ( LHRC).
Picha ya Pamoja ya washiriki wote katika maadhimisho maadhimisho ya miaka 115 ya Siku ya Wanawake Duniani.




































.jpg)