Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackon (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran nchini Tanzania Mhe. Hossein Alvandi Bahineh, alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo Mei 30, 2022 kwa lengo la kujitambulisha.