Featured Kitaifa

DKT. KIRUSWA KUSHIRIKI MKUTANO WA UWEKEZAJI RASILIMALI ZA MADINI, NISHATI NIGERIA

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa na Watalaam kutoka Wizarani wanatarajia kushiriki Mkutano wa Uwekezaji katika Rasilimali za Madini na Nishati utakaofanyika kuanzia tarehe 31 Mei hadi 3 Juni, 2022 nchini Nigeria.

Leo Mei 30, Naibu Waziri Dkt.Kiruswa amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Benson Bana ambaye amemweleza kuhusu nia ya Mfanyabiashara mkubwa wa nchini humo Aliko Dangote kuwekeza katika kiwanda kikubwa cha mbolea nchini.

About the author

mzalendoeditor