Featured Kitaifa

MBARONI KWA KUMUIBA MTOTO WA MIEZI MITATU

Written by mzalendoeditor

JESHI la Polisi Mkoani Geita linamshikilia Mariamu Samuel (21) Mkazi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro Wilayani Geita kwa tuhuma za kumuiba mtoto mdogo wa miezi mitatu katika Kijiji cha Marerani Kata ya Ludete mkoani humo.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Henry Mwaibambe, amesema Mariamu alifika kwenye kijiji hicho na kumrubuni Catherine Michael mwenye umri wa miaka 4 ambaye alikuwa amembeba mtoto mwenzake na kumwambia amwachie mtoto huyo kisha akamtuma Catherine maandazi na aliporudi hakumkuta Mariamu wala mtoto.

“Baada ya kupata taarifa za kuibiwa kwa mtoto huyo, Polisi walifanya msako na kumkamata Mariamu akiwa na Mtoto huyo katika Kijiji Cha Nyantimba Wilayani Chato na kumchukua Mtoto huyo kumkabidhi mama yake, Mariamu bado anashikiliwa kwa upelelezi pindi ushahidi utakapokamilika atafikishwa Mahakamani”

About the author

mzalendoeditor