Featured Michezo

MORRISON AIBEBA SIMBA CAF,ASEC MIMOSAS YAIFANYIA MAUAJI RSB BERKANE

Written by mzalendoeditor

Na.Alex Sonna

Winga mtukutu wa klabu ya Simba Bernard Morrison ameibeba mabegani timua yake baada ya kutokea benchi na kwenda kusawazisha bao na kuondoka na Pointi moja na kuwafanya waongoze kundi D.

Huo ulikuwa mchezo wa pili wa Simba katika Kombe la Shirikisho barani Afrika umeipa nguvu baada ya sare ya kufungana bao 1-1 na  wenyeji US Gendarmerie mchezo uliopigwa katika kwenye Uwanja wa Général Seyni Kountché, Niamey nchini Niger.

Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Gbeuli Wilfried dakika ya 11 na Simba walipata bao kupitia kwa Bernard Morrison akifunga kwa kichwa mpira wa Kona uliopigwa na Shomari Kapombe dakika ya 84.

Kwa matokeo hayo Simba wanaongoza kundi D kwa kufikisha pointi 4 baada ya RSB Berkane kufungwa mabao 3-1 na Asec Mimosas na sasa nafasi ya pili inashikwa na Asec Mimosas wakiwa na Pointi 3 sawa na RSB Berkane wakiwa nafasi ya tatu huku US Gendarmerie wakiburuza mkia wakiwa na Pointi moja.

Simba watashuka tena uwanja Februari 27 kucheza na RSB Berkane mchezo utakaopigwa nchini Morocco.

About the author

mzalendoeditor