Kitaifa Makala

ATELEKEZA FAMILIA MIAKA 12 BAADA YA MKE WAKE KUJIFUNGUA MTOTO MLEMAVU.

Written by mzalendoeditor

Na: Rose Jacob,Mwanza.

Mwanamke Anchila Emiliani ambaye ni mama mzazi wa mtoto Geofray Godwin aliyepo pichani mkazi wa  Mtaa wa Kilimahewa Jijini Mwanza amesema kuwa alitelekezwa na mume wake  baada ya kujifungua  mtoto mwenye ulemavu wa Viungo na akili hadi sasa ni miaka kumi na mbili bila kuonana naye.

Akizungumza na  nyumbani kwake, Anchila Emiliani amesema kuwa baada ya mume wake kuitelekeza familia hiyo alisababisha hali ya familia hiyo kuwa duni kiuchumi na kuishi kwa tabu.

Akifafanua baada ya kukabidhiwa msaada wa vitu mbali mbali vilivyotolewa na wadau kupitia Nitetee Faundation na taasisi ya Desk and Chair,amesema mume wake alimkimbia na kumuacha  mtoto wake huyo akiwa na umri wa miaka saba na mpaka leo  ni miaka 19 bila kumuona.
“Nilivyo mzaa Geofray nilipoteza fahamu nilipozinduka daktari aliniambia mwanangu ana matatizo lakini tulipata matibabu na kuruhusiwa baada ya miezi sita nilipo mpeleka Kliniki niligundua kuwa mtoto wangu ni mlemavu,”alisema Anchila.

Alisema kutokana na hali hiyo mwanaume aliondoka na maisha yakabadilika yakawa ni ya mateso,alimuacha akiwa na watoto wawili ambaye ni Geofray na mdogo wake kwa sasa ana umri wa miaka 17 yuko kidato cha tatu.
Ameongeza kuwa walikosa mahala pa  kuishi,uangalizi wa mtoto ukawa mbaya,kufuatia kumuacha mtoto huyo na kwenda kuhangaika kutafuta chakula kwa ajili ya kuhudumia familia hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Nitetee Faundation Frola Lauo,aliomba Serikali kuhakikisha watendaji wa ustawi wa jamii hawakai maofisini,bali watoke na kuangalia hali za maisha ya watoto walioko majumbani,maana wazazi wengine wanawafungia watoto ndani kwa kuogopa fedhea pindi watakapo bainika na kuletewa misaada.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimahewa Amini Fataki na mhudumu wa afya ngazi ya jamii Mwajuma Mlekwa, walisema maisha ya mtoto Geofray ni ya tabu sana maana anaishi kwa kunywa kijiko kimoja cha maji au chai ambacho kinachukua dakika tano kukimeza maana kwenye koo lake kuna vitu kama nyama,hivyo wanawaomba watu mbali mbali waendelee kujitokeza kumchangia gharama za matibabu ili atibiwe,ingawa tayari fedha za kumkatia bima zimeisha patikana

About the author

mzalendoeditor