Mkuu wa taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Arusha James Ruge akiongea na waandishi wa habari
…………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa mkoa wa Arusha(TAKUKURU) imewatahadharisha wananchi juu ya uwepo wa matapeli wanaotumia jina la taasisi hiyo ili kuweza kujipatia fedha.
Akitoa taarifa ya taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Arusha James Ruge alisema kuwa ni vema wananchi wakajiridhisha na wito wowote wa simu kwa kufika ofisi ya TAKUKURU iliyo karibu.
“Epukeni kutoa fedha kwani huduma zetu haziuzwi, unapopata wito wowote wa simu kuwa jaribu kujiridhisha kwa kufika katika ofisi zetu zilizo karibu,” Alisema Ruge.
Aidha alisema kuwa kwa muda wa miezi mitatu taasisi hiyo imefuatilia miradi 17 yenye thamani ya bilioni 7.8 na kubaini kasoro mbalimbali ambapo baadhi wameshauri kurekebishwa na zingine uchungu umeanzishwa.
Alisema miradi hiyo ni pamoja na miradi saba ya barabara katika Jiji la la Arusha, wilaya ya Arumeru, Longido, Monduli na Ngorongoro ambapo miradi miwili ya Monduli ilibainika kuwa na kasoro, miradi miwili ya maji halmashauri ya Monduli na mmoja ulikutwa na kasoro na yote imetolewa ushauri wa kurekebisha kasoro husika.
Alifafanua kuwa miradi mingine waliyofuatilia ni miradi mitano ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule za sekondari Monduli, Karatu na Longido, ambazo taratibu za kumpata mkandarasi hazikufuatwa katika ujenzi wa darasa wilayani Monduli ambapo uchunguzi umeanzishwa.
“Mradi mwingine ni mradi afya wa ujenzi wa nyumba za watumishi katika halmashauri ya wilaya ya Monduli na ujenzi wa jengo la OPD katika wilaya ya Karatu ambapo katika nyumba ya watumishi tumebaini kuwa na kasoro katika taratibu za kutafuta mkandarasi na tumeanzisha uchunguzi,” Alisema Ruge.
Alifafa nua katika miradi ya kilimo na mifugo katika ujenzi wa josho la mifugo wilaya ya Longido na Karatu wamepaini kasoro Longido na wameanzisha uchunguzi.
Sambamba na hayo pia amesema kuwa wamefanya uchambuzi wa mfumo wa utendaji wa kazi wa wakala wa huduma za umeme na ufundi ( TEMESA)mkoani Arusha ambapo wamegundua uchelewaji wa huduma ya matengenezo ya magari ya utolewaji wa huduma hafifu kwa wateja na kuaazimia mapungufu husika yarekebishwe.
“Tumefanya uchambuzi wa mfumo wa usimamizi wa mapato yatokanayo na ushuru wa madini ya ujenzi katika wilaya ya Arumeru na Ngorongoro ambapo tumegindua kutokuwepo kwa leseni kwenye baadhi ya machimbo na kutofanyika kwa kaguzi za mazingira katika baadhi ya machimbo,”Alieleza.
Hata hivyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi wamepokea taarifa 114 kati yake 91 zikiwa zinahusu Rushwa na 23 zilihusu makosa mengine ambapo
Majalada 63 uchunguzi unaendelea na 28 uchunguzi umekamilika.