Featured Kitaifa

KAMATI YA KUKUSANYA MAONI YA WANANCHI NGORONGORO YAWASILISHA TAARIFA  KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU

Written by mzalendoeditor
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kukusanya maoni na mapendekezovya wananchi wa tarafa ya Ngorongoro na tarafa ya Sale.
Diwani wa kata ya a Nainokanoka wilaya ya Ngorongoro  Edward Maura ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kukusanya maoni na mapendekezo ya wananchi wa tarafa ya Ngorongoro na tarafa ya Sale akionyesha ripoti waliyoipeleka katika ofisi ya waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Mwenyekiti wa kamati ya kukusanya maoni na mapendekezo ya wananchi wa tarafa ya Ngorongoro na tarafa ya Sale akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha juu ya ripoti walioiwasilisha Ofisi ya waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania
……………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Kamati ya kukusanya maoni na mapendekezi ya wananchi katika Tarafa ya Ngorongoro, Sale na Loliondo umewasilisha taarifa ya  kukusanya maoni  na  mapendekezo kwa wananchi na kuwasilisha katika Ofisi ya Waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano kwa lengo la kupata suluhu kutoka serikalini.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha Mwenyekiti wa kamati hiyo Metui Sheudo alisema mchakato huo wa mapendekezo ya wananchi umedumu kwa muda wa miezi mitatu ikiwa lengo ni kuwafikia wananchi katika kata zote na kutoa maoni na mapendekezo yao.
“Tunatumaini mapendekezo haya serikali itatoa matokeo chanya kwa ajili ya ustawi wa wananchi wa Ngorongoro na utaleta suluhu katika utatuzi wa migogoro ya ardhi katika eneo lenye kilometa za mraba 1500 bila kuathiri pande zote mbili,”alisema Mwenyekiti huyo.
Metui alisema hatua hiyo ilifuata baada ya mchakato wa kuwashirikisha wananchi na makundi mbalimbali katika jamii kuwa hafifu katika kutatua mgogoro huo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Nainokanoka Edward Maura alisema wanaishukuru serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu kwa kutoa fursa kwa wananchi wa wilaya ya Ngorongoro kuunda kamati na kuandika mapendekezo ya jamii juu ya mwenendo wa changamoto zilizopo wilayani hapo.
“Na kupitia kamati iliyokuwa na wajumbe wa pande zote katika jamii tumeikamilisha hiyo kazi kutokana na ushirikiano baina ya wananchi na wanakamati hali iliyoleta tija katika kuandika taarifa hiyo tuliyoiwasilisha serikalini,”alisema Maura 
Pia alisema wanamshukuru waziri mkuu kwa kupokea taarifa hiyo na kuwaahidi serikali kupitia Mbunge wa Ngorongoro kurudi kwa ajili ya majadiliano  hivyo wanategemea taarifa hiyo kutoa mateokeo chanya.
Naye Magreth Kaisoi mwanakamati wa kamati ripoti hiyo Alieleza kuwa ripoti hiyo imeeleza ukweli halisi kuhusu Ngorongoro ambapo serikali ikiisoma itaweza kujua ukweli ni kwajinsi gani uhai wa Ngorongoro bado upo.

About the author

mzalendoeditor