Featured Kitaifa

WAZIRI CHONGOLO AZINDUA BODI YA MAKAMISHNA WA  TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA

Written by Alex Sonna

WAZIRI  wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo,akizungumza wakati akizindua rasmi bodi ya Makamishna wa  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, katika hafla iliyofanyika leo Januari 30,2026 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo,akizungumza wakati akizindua rasmi bodi ya Makamishna wa  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, katika hafla iliyofanyika leo Januari 30,2026 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo,akizungumza wakati akizindua rasmi bodi ya Makamishna wa  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, katika hafla iliyofanyika leo Januari 30,2026 jijini Dodoma.

MWAKILISHI wa Katibu Mkuu Wizara ya  Kilimo, Bw.James Kibamba ,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi ya Makamishna wa  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, katika hafla iliyofanyika leo Januari 30,2026 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Makamishna wa TCDC, Bw. Abdul Majid Nsekela,akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo,kuzindua bodi ya Makamishna wa  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, katika hafla iliyofanyika leo Januari 30,2026 jijini Dodoma.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege ,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi ya Makamishna wa  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, katika hafla iliyofanyika leo Januari 30,2026 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Waziri   wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (hayupo pichani)  wakati akizindua rasmi bodi ya Makamishna wa  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, katika hafla iliyofanyika leo Januari 30,2026 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo,akiwa katika picha ya pamoja mara kuzindua bodi ya Makamishna wa  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, katika hafla iliyofanyika leo Januari 30,2026 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo,akiwa katika picha ya pamoja mara kuzindua bodi ya Makamishna wa  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, katika hafla iliyofanyika leo Januari 30,2026 jijini Dodoma.

Alex Sonna-DODOMA


WAZIRI  wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo, ameielekeza Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kusimamia kwa umakini maeneo muhimu yatakayochochea maendeleo ya vyama vya ushirika na kukuza uchumi wa wananchi kupitia mfumo wa ushirika.

Mhe. Chongolo,ameyasema hayo,wakati akizindua rasmi bodi ya Makamishna wa  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, katika hafla iliyofanyika leo Januari 30,2026 jijini Dodoma.

 Waziri Chongolo ametaja maeneo yanayopaswa kupewa kipaumbele kuwa ni pamoja na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na mizani za kidijiti katika vyama vya ushirika, ili kuongeza uwazi na kupata takwimu sahihi kwa manufaa ya wanachama.

Maeneo mengine ni pamoja na kufanya ukaguzi wa kila mwaka kwa vyama vyote vya ushirika nchini, utafutaji wa masoko ya nje kwa bidhaa za vyama hivyo, uwekezaji sahihi wa mali za vyama pamoja na kuimarisha uongozi wenye maadili na watendaji wenye sifa stahiki.

 “Umuhimu wa Kamisheni hiyo ni kusimamia kwa karibu utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  kupitia mfumo wa ushirika, akitaja ujenzi wa viwanda, upatikanaji wa bima ya mazao, huduma za matibabu pamoja na mafao ya uzeeni kwa wakulima kama maeneo muhimu yanayotarajiwa kutekelezwa.”amesisitiza Waziri Chongolo

Hata hivyo  Mhe. Chongolo ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Kamisheni hiyo ili kuhakikisha sekta ya ushirika inaendelea kukua na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Aidha, Waziri Chongolo ameipongeza Kamisheni iliyomaliza muda wake chini ya Mwenyekiti wake, Ndg. Abdulmajid Nsekela, kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ikiwemo kuboresha taswira ya ushirika nchini, kuanzishwa kwa Benki ya Ushirika pamoja na maboresho ya Sheria ya Ushirika.

 Pia Waziri Chongolo amempongeza Ndg. Abdulmajid Nsekela kwa kuteuliwa tena kuiongoza Kamisheni hiyo kwa awamu ya pili, huku akitoa wito kwa wajumbe wapya kuweka mikakati thabiti itakayosaidia kuleta matokeo ya haraka na kuimarisha imani ya wananchi katika vyama vya ushirika.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Makamishna wa TCDC, Bw. Abdul Majid Nsekela, amesema bodi hiyo ipo tayari kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Serikali kwa kushirikiana na menejimenti ya Tume, akisisitiza kuwa bodi itaweka mikakati madhubuti ya kuimarisha vyama vya ushirika nchini.

“Tunatambua dhamana tuliyopewa na Serikali, na tutaifanyia kazi kwa weledi, uwazi na uadilifu ili kuleta mageuzi ya kweli kwenye sekta ya ushirika.”amesema Bw.  Nsekela

Naye Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege, amesema Tume itaendelea kusimamia vyama vya ushirika kwa kuzingatia matumizi ya TEHAMA, ukaguzi wa mara kwa mara na uimarishaji wa uongozi ili kuhakikisha maslahi ya wanachama yanalindwa.


“Tutahakikisha vyama vinaendeshwa kwa misingi ya uwajibikaji na vinaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya wakulima na wananchi kwa ujumla.”amesema Dkt. Ndiege

About the author

Alex Sonna