Featured Kitaifa

RAIS SAMIA KUSHIRIKI MDAHALO WA WAKUU WA NCHI, ACCRA NCHINI GHANA

Written by mzalendoeditor

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama na Rais wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo, Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika Mdahalo pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa nchi nyingine kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB kujadili fursa mbalimbali pamoja na changamoto zinazolikabili Bara la Afrika. Mkutano huo wa 57 wa AfDB unafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022. Wa kwanza kushoto ni Rais wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo pamoja na Makamu wa Rais wa Ivory Coast Mhe. Tiémoko Meyliet Koné Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama na Rais wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo, Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina pamoja viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja mara baada ya  ufunguzi wa Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022. 

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022.

************************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema licha ya hali ya uchumi kushuka wakati anaingia madarakani kutokana na janga la UVIKO 19 kuathiri uchumi wa dunia, uchumi wa Tanzania kwa sasa unaimarika.

Mhe. Rais Samia amesema hayo wakati akijibu swali katika Mdahalo wa Wakuu wa Nchi uliojadili fursa zilizomo na changamoto zinazozikabili Nchi za Afrika uliofanyika Accra, Ghana katika Mkutano wa 57 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Aidha, Mhe. Rais Samia amesema wakati wa janga la UVIKO 19 uchumi wa nchi ulishuka kutoka asilimia 6.4 hadi asilimia 4 lakini kwa sasa umekuwa na kufikia asilimia 5.2 kwa mwaka huu huku matarajio ni kufikia asilimia 6.7 mwaka 2025.

Vile vile, Rais Samia amesema AfDB na Mashirika ya Kimataifa yamechangia kuendeleza kilimo, miundombinu ya barabara pamoja na viwanja vya ndege, hivyo kusaidia kuunganisha Tanzania na nchi jirani.

Rais Samia pia amesema kutokana na janga la UVIKO 19, Shirika la Fedha Duniani (IMF) liliipatia Tanzania Mkopo wa kukabiliana na janga hilo ambapo Tanzania ilitumia fedha hizo katika sekta ya Elimu, maji pamoja na afya.

Aidha, Rais Samia amesema fedha za UVIKO 19 zimesaidia kusambaza maji katika maeneo ya mijini na vijijini ambapo hadi kufikia mwaka 2025 anatarajia usambazaji wa maji maeneo ya vijijini kuwa asilimia 85 na asilimia 95 kwa maeneo ya mijini.

About the author

mzalendoeditor