Featured • Kitaifa

ELIMU YA UDHIBITI YAWAFIKIA WENYE ULEMAVU TABORA

Written by Alex Sonna

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi,Mhandisi Karim Ally, akitoa elimu kwa wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu ( SHIVYAWATA) mkoa wa Tabora leo Oktoba 6,2026.

Na Mwandishi Wetu,TABORA

Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi, leo, tarehe 6/10/2026, imekutana na wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kwa mkoa wa Tabora, na kuwaelimisha kuhusu haki na wajibu wao katika huduma za nishati na maji.

Wanachama hao pia wamepata elimu kuhusu utaratibu wa kuwasilisha malalamiko na namna yanavyoshughulikiwa, kanuni za ubora wa huduma ya maji, matumizi sahihi na salama ya gesi ya kupikia na umuhimu mikataba ya huduma kwa wateja huku wakisisitizwa kutumia mafundi umeme wenye leseni zilizotolewa na EWURA.

Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Karim Ally, akifungua warsha hiyo iliyofanyika katika Ofisi za EWURA Kanda ya Magharibi, mjini Tabora, ameeleza kuwa ni utaratibu wa Mamlaka kukutana na wadau mbalimbali ikiwemo watu wenye ulemavu ili kuwaelimisha kuhusu udhibiti sanjari na kupokea mrejesho kuhusu huduma zinazodhibitiwa.

Aidha, washiriki wameiomba EWURA kuendeleza elimu hiyo kwa kuwafikia wanachama wa SHIVYAWATA katika maeneo mbalimbali nchini na pia kwa makundi mengine ya aina hiyo ili kuimarisha uelewa wao katika masuala ya kiudhibiti.

 Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi,Mhandisi Karim Ally, akitoa elimu kwa wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu ( SHIVYAWATA) mkoa wa Tabora leo Oktoba 6,2026.

 Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi,Mhandisi Karim Ally, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa  elimu kwa wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu ( SHIVYAWATA) mkoa wa Tabora leo Oktoba 6,2026.

About the author

Alex Sonna