Featured Kitaifa

NINDIE: WAKAGUZI WA NDANI WAIMARISHE USIMAMIZI WA VIHATARISHI

Written by Alex Sonna

 

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie, akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani, kwa ngazi ya Utawala, ulioandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa ndani Tanzania (The Institute of Internal Auditors- Tanzania), uliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). 

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika, CPA. Alphonce Muro, kabla ya kufunga Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani pamoja na Jukwaa la 13 la Utawala Bora, ulioandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa ndani Tanzania (The Institute of Internal Auditors- Tanzania), uliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).  

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (kulia), pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Juma Kaniki, wakifuatilia Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani pamoja na Jukwaa la 13 la Utawala Bora, ulioandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa ndani Tanzania (The Institute of Internal Auditors- Tanzania), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (kulia), akiteta jambo na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Juma Kaniki, wakati wa Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani pamoja na Jukwaa la 13 la Utawala Bora, ulioandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa ndani Tanzania (The Institute of Internal Auditors- Tanzania), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). 

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie, akifuatilia Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani pamoja na Jukwaa la 13 la Utawala Bora, ulioandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa ndani Tanzania (The Institute of Internal Auditors- Tanzania),  uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), ulioandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa ndani Tanzania (The Institute of Internal Auditors- Tanzania).

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Msaidizi, Sehemu ya Udhibiti Ubora, Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bw.  Ng’wanzalima John (kushoto) pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Msaidizi, Wizara ya Fedha, Bw. Paison Mwamnyasi, wakiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani pamoja na Jukwaa la 13 la Utawala Bora, ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo.

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Msaidizi, Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Paison Mwamnyasi, akifuatilia Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani pamoja na Jukwaa la 13 la Utawala Bora, ulioandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa ndani Tanzania (The Institute of Internal Auditors- Tanzania), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).  

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha, wakifuatilia Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani pamoja na Jukwaa la 13 la Utawala Bora, ulioandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa ndani Tanzania (The Institute of Internal Auditors- Tanzania), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).  

Picha za matukio mbalimbali wakati wa kufunga Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani, ngazi ya Utawala, ulioandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa ndani Tanzania (The Institute of Internal Auditors- Tanzania), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).  

(Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, WF – Arusha)

Na. Asia Singano, WF -Arusha.

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa vihatarishi pamoja na kujenga uwezo wa wataalam wa ukaguzi wa ndani ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika taasisi za umma.

Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa 19 wa Ukaguzi kwa ngazi ya utawala, Mhandisi Nindie alisema, kuimarika kwa usimamizi wa vihatarishi kunahitaji mifumo madhubuti, uendelezaji wa ujuzi na matumizi ya fursa za mafunzo yanayopatikana, ikiwemo mafunzo yanayotolewa kwa njia ya mtandao.

Alisema Wizara ya Fedha inatambua umuhimu wa kuendelea kutoa mafunzo kwa wakaguzi wa ndani yatakayowawezesha wataalam kuongeza ujuzi wao, hatua inayoweza kusaidia kuimarisha uwezo wa taasisi katika kutambua na kudhibiti vihatarishi.

‘’Tunategemea kuwa na mafunzo kwa njia ya mtandao ili kuongeza uwezo wa wakaguzi wa ndani, na kwa wakaguzi ambao tumeshiriki na tupo basi mijadala hii ambayo imeendelea jana na leo itusaidie kuona kuwa Bodi zetu zinahitaji tufanye nini lakini taasisi kufikia malengo ambayo tumejiwekea hasa kuhakikisha thamani ya mali za umma inapatikana kwa wananchi ambao tunawatumikia’’alisema Mhandisi Nindie.

Alisema ushirikiano kati ya bodi, menejimenti, wakaguzi wa ndani na wadau wengine ni muhimu katika kuhakikisha mapendekezo yanayotokana na ukaguzi yanafanyiwa kazi na kusaidia kuboresha utendaji wa taasisi.

‘’Tutaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wote katika kuimarisha mifumo ya ukaguzi wa ndani lakini usimamizi wa vihatarishi ili kuongeza tija na ufanisi kwa lengo moja kubwa la kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika kwa tija ili kuchagia maendeleo ya Taifa’’ alisema Mhandisi Nindie.

Katika mkutano huo viongozi mbalimbali wa Wizara ya Fedha, walishiriki akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda.  
Katika mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani kwa ngazi ya Utawala ambao umehitimishwa rasmi ambapo washiriki walipata fursa ya kujadiliana kubadilishana uzoefu pamoja na mafunzo mbalimbali ikiwemo matumizi ya teknolojia hususan matumizi ya Akili Unde (AI), huku wakisisitizwa kushiriki katika kujadili na kusimamia hatari na athari za teknolojia hiyo kabla ya kuangalia manufaa yake pekee.

About the author

Alex Sonna