Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, akiongoza kikao kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Ujumbe wa Benki ya Dunia, kilichofanyika, Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, kilicholenga kuhitimisha maandalizi ya kitaalamu ya Programu ya Uendelezaji wa Ushoroba wa Kati wa Maendeleo ya Kiuchumi Utakaoongeza Ajira kwa Vijana (KAZI MPA).
Na. Josephine Majura na Asia Singano, WF – Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, ameongoza Ujumbe wa Serikali ya Tanzania kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, katika kikao na Ujumbe wa Benki ya Dunia kilicholenga kuhitimisha maandalizi ya kitaalamu ya Programu ya Uendelezaji wa Ushoroba wa Kati wa Maendeleo ya Kiuchumi Utakaoongeza Ajira kwa Vijana (CATALYZING JOBS AND RESILIENT GROWTH IN THE CENTRAL CORRIDOR MULTIPHASE PROGRAMMATIC APPROACH
(KAZI MPA).
Kikao hicho kilifanyika kwa lengo la kuwasilisha na kujadili matokeo ya maandalizi yaliyofanywa kwa pamoja kati ya Serikali na Benki ya Dunia, pamoja na kukubaliana hatua zinazofuata kuelekea kukamilisha maandalizi ya Programu hiyo, kilichofanyika, Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Katika kikao hicho, pande hizo zilijadili kwa kina maeneo muhimu ya utekelezaji wa KAZI MPA, huku zikisisitiza umuhimu wa programu hiyo katika kuchochea mageuzi ya kiuchumi, kuongeza uwekezaji na kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa Tanzania.
Aidha, KAZI MPA inalenga kuongeza fursa za ajira, hususan kwa vijana, pamoja na kuimarisha ushindani wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa kupitia kuendeleza miundombinu na mazingira wezeshi ya shughuli za kiuchumi katika Ushoroba wa Kati.
Utekelezaji wa programu hiyo unatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya jitihada za Serikali katika kutafsiri kwa vitendo malengo ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050, hususan katika kujenga uchumi wenye tija, jumuishi na stahimilivu, unaotoa fursa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na biashara.
Ujumbe wa Serikali katika kikao hicho uliwahusisha pia Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw. Adolf Ndunguru, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvivu Bi. Agness Meena, Kaimu Katibu Mkuu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Nsubil Joshua, Naibu Makatibu Wakuu Wizara ya Kilimo, Prof. Peter Msoffe na Mhandisi Athumani Kilundumya pamoja na Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Taifa ya Mipango Bw. Sosthenes Kewe.
Kwa upande wa Ujumbe wa Benki ya Dunia ukiongozwa na Meneja wa Benki ya Dunia, Kitengo cha Utekelezaji wa Sekta ya Usafiri, Afrika Mashariki na Kusini, (Practice Manager for Transport in Eastern and Southern Africa), Bw. Binyam Reja.
Kikao hicho ni hatua muhimu kuelekea kukamilisha maandalizi ya KAZI MPA na kuweka msingi wa utekelezaji wa programu inayolenga kuchochea shughuli za kiuchumi, kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika uchumi wa kikanda na kimataifa.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, akiongoza kikao kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Ujumbe wa Benki ya Dunia, kilichofanyika, Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, kilicholenga kuhitimisha maandalizi ya kitaalamu ya Programu ya Uendelezaji wa Ushoroba wa Kati wa Maendeleo ya Kiuchumi Utakaoongeza Ajira kwa Vijana (KAZI MPA).
Meneja wa Benki ya Dunia, Kitengo cha Utekelezaji wa Sekta ya Usafiri, Afrika Mashariki na Kusini, (Practice Manager for Transport in Eastern and Southern Africa), Bw. Binyam Reja, akizungumza wakati wa kikao na Ujumbe wa Serikali ya Tanzania uliyoongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, (hayupo pichani), kilichofanyika Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Baadhi ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, wakifuatilia kikao kilichohusisha Ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Ujumbe wa Benki ya Dunia, kilichofanyika, Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, kilicholenga kuhitimisha maandalizi ya kitaalamu ya Programu ya Uendelezaji wa Ushoroba wa Kati wa Maendeleo ya Kiuchumi Utakaoongeza Ajira kwa Vijana (KAZI MPA).
(Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, WF – Dodoma)


.jpg)
.jpg)