Featured Kitaifa

MSD YAIBUKA KINARA KATIKA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST

Written by Alex Sonna

Bohari ya Dawa (MSD) imeendelea kuthibitisha ubora wake katika usimamizi wa ununuzi wa umma baada ya kutunukiwa Tuzo ya Utendaji Bora katika Ununuzi wa Umma* na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

MSD imetambuliwa kama Taasisi Bora kwa Ujumla katika Matumizi ya Mfumo wa Kitaifa wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Kielektroniki (NeST) kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni uthibitisho wa uwazi, ufanisi na matumizi sahihi ya teknolojia katika utekelezaji wa shughuli za ununuzi wa umma.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa hapo jana tarehe 29 Julai 2026, wakati wa Kongamano la 10 la Kitaifa la Ununuzi wa Umma, linaloendelea katika Ukumbi wa AICC, Mkoani Arusha.

About the author

Alex Sonna