Featured Kitaifa

ELIMU NJE YA MFUMO RASMI KUENDELEA KUPANULIWA KUONGEZA FURSA KWA VIJANA

Written by Alex Sonna

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda,  akiwasilisha Hotuba ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 leo Mei 7,2026  bungeni Dodoma.

Na.Alex Sonna,Mzalendo blog-DODOMA

Serikali imeendelea kuimarisha elimu nje ya mfumo rasmi ili kuhakikisha vijana na watu wazima zaidi wanapata fursa ya kupata elimu, ujuzi na stadi za maisha zinazowawezesha kujiajiri na kuajiriwa.

Kupitia mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio Nje ya Mfumo Rasmi, Serikali inalenga kuongeza idadi ya wanufaika kutoka vijana 16,732 mwaka 2026 hadi 22,500 mwaka 2027.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof Adolf Mkenda wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2026-2027.

Amesema elimu nje ya mfumo rasmi inalenga kuwasaidia wale waliokosa nafasi katika mfumo rasmi wa elimu kutokana na sababu mbalimbali, ili waweze kupata maarifa na stadi za maisha kulingana na mahitaji ya jamii na soko la ajira.

About the author

Alex Sonna