
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange ambaye ni Mwenyekiti Mwenza akizungumza wakati wa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar Februari 16, 2026. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe. Hamza Hassan Juma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe. Hamza Hassan Juma ambaye ni Mwenyekiti akizungumza wakati wa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar Februari 16, 2026. Kushoto kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange.

Wajumbe wakishiriki kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar Februari 16, 2026.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange ambaye ni Mwenyekiti Mwenza (kulia) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe. Hamza Hassan Juma kabla ya kuanza kwa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar Februari 16, 2026.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe. Hamza Hassan Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar Februari 16, 2026. Viongozi wengine pichani ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dkt. Islam Seif Salum (kulia), Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Salhina Mwita Ameir (kushoto).
……
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange ametoa rai kwa watendaji kulipa umuhimu suala la Uchumi wa Buluu kuwa sehemu ya agenda katika vikao vya pande mbili za Muungano.
Amesema hayo wakati wa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar Februari 16, 2026.
Dkt. Dugange alisema kuwa Zanzibar imepiga hatua katika eneo la uchumi hivyo kuendeleza ushirikiano wake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaimarisha uchumi wa Taifa.
Alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais tayari imeanzisha Kitengo cha Usimamizi wa Uchumi wa Buluu ambacho ni fursa adhimu kwa wananchi kupata uelewa kuhusu sekta hiyo kupitia elimu inayotolewa.
Aidha, Naibu Waziri alisema kuwa ni muhimu kuzungumzia zaidi fursa zinazopatikana katika Muungano ikiwemo miradi mbalimbali inayotekelezwa katika pande zote mbili hatua itakayowawezesha kuzichangamkia na hivyo kuinua kipato na uchumi wa nchi.
Pamoja na mambo mengine, aliongeza kuwa Muungano umekuwa ni chachu ya uchumi kwakuwa umeimarisha mazingira kupitia miradi ya maendeleo ikiwemo biashara ya kaboni ambayo inafanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo misitu na hata bahari.
“Tuwapongeze viongozi wetu wa kitaifa yaani Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuimarisha huduma za kijamii na miundombinu, yote hii ni katika kuwanuia wananchi wa pande zote mbili za Muungano,” alisema.
Kwa upande Wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe. Hamza Hassan Juma alishauri elimu ya Muungano iendelee kutolewa hususan kwa kundi la vijana.
Alishauri kuwatumia wasanii mbalimbali nchini katika kutoa elimu ya Muungano, kwani wengi wao ni vijana hatua itakayoisaidia kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi katika kundi hilo.
Halikadhalika, Mhe. Hamza alitoa rai kwa watendaji kutoka Ofisi hizo mbili kutangaza zaidi fursa zinazopatikana katika Muungano badala ya changamoto akisema kuwa Serikali zote zinazishughulikia ili kuzimaliza.
Waziri Hamza pia, alitumia nafasi hiyo kupongeza juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimamia sekta ya uchumi ambao umeendelea kuimarika siku hadi siku kwa maendeleo endelevu.
Awali viongozi hao wawili walikutana na kufanya mazungumzo na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa Serikali hizo mbili katika kuulinda na kuuenzi Muungano kwa manufaa ya wananchi wananchi.
Naibu Waziri Dkt. Dugange alipongeza kazi kubwa ya maendeleo inayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) chini ya Rais Dkt. Mwinyi ikiwemo miundombinu ikiwemo madaraja ya juu (flyover), uwanja wa ndege na bandari zmbayo itasaidia wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanis.
Vilevile, alisema kuwa kupitia maendeleo hayo kipato cha mtu mmoja mmoja na uchumi wa Zanzibar unakua akiongeza kuwa hayo ndio matunda ya Muungano.
Kwa upande wake Waziri Hamza alitoa rai kwa watendaji kutangaza zaidi fursa za zinazopatikana katika Muungano badala ya changamoto kwani tayari viongozi wa Serikali zote mbili wanaendelea kuzitatua.