Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya mawasiliano ya YAS kwa kushirikiana na Mixx, imezindua rasmi maandalizi ya mbio za Yas Zanzibar International Marathon 2025.
Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Novemba 23, visiwani Zanzibar, zikiongozwa na kauli mbiu isemayo “Kila Hatua ni Special.”
Meneja wa Mawasiliano YAS, Bi. Christina Murimi, amesema lengo kuu ni kuhamasisha afya, utalii na maendeleo ya jamii.
Amesema mbio hizo zitaendeshwa kwa njia za 5KM, 10KM na 21KM, huku usajili ukifanyika kidigitali kupitia mfumo wa Mixx.
Kwa upande wake, kiongozi wa mbio hizo Bw. Ali Said amesema tukio hilo linawaleta pamoja watu wa rika na tabaka mbalimbali.
Amesisitiza kuwa mbio hizo si michezo tu, bali ni fursa ya kukuza utamaduni, teknolojia na utalii wa Zanzibar.
YAS imehimiza wananchi kujisajili mapema na kushiriki kwa wingi ili kuwa sehemu ya tukio la kihistoria visiwani humo.