Featured Kitaifa

WAHITIMU WA MAFUNZO YA MFUMO WA STAKABADHI GHALA WASISITIZWA KUZINGATIA UWAZI

Written by mzalendoeditor
Mwenyekiti  wa Kamati ya Huduma ya Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,Godwin Mkanwa,akikabidhi Cheti Mhitimu bora wa  mafunzo ya mfumo wa Stakabadhi Ghala  kuelekea Msimu wa mazao ya Mbaazi na Dengu 2025-2026 yaliyomalizika leo Juni 28,2025 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MWENYEKITI wa Kamati ya Huduma ya Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,Godwin Mkanwa,ameagiza mambo manne kwa wahitimu wa mafunzo ya mfumo wa Stakabadhi ghalani ikiwemo kufanya kazi  kwa uwazi,tija na ufanisi ili kuweka imani kwa wakulima.
Maagizo hayo ameyatoa leo Juni 28,2025 Jijini Dodoma  wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa Stakabadhi Ghala  kuelekea Msimu wa mazao ya Mbaazi na Dengu 2025-2026.
Mkanwa  amewataka wahitimu hao kuongeza uwazi na ubora katika utendaji kazi wao ambapo amedai mfumo huo ni madhubiti katika  kuondoa dhulma na kurasimisha biashara ya wakulima.
Pia  amewataka kushughulikia  udanganyifu kwa kuhakikisha haukubaliki katika jamii ya wakulima.
Aidha,amesema katika kukabiliana na jambo hilo,wamefunga  CCTV Camera katika kila Ghala lengo likiwa ni kuondoa udanganyifu ambapo amedai wale ambao watawabaini watawachukulia hatua kali za kisheria.
Mkanwa  amesema mfumo wa Stakabadhi Ghalani umemsaidia mkulima kupata bei nzuri huku akitoa wito kwa wasimamizi hao kuwa walinzi na waadilifu katika kila walichofundishwa.
“Toeni taarifa kwa uwazi jukumu lenu kutunza Imani ya wakulima na wadau,mkitoa taarifa kwa uwazi ili tutunze Imani ya watu wetu,”amesema Bw.Mkanwa
Kwa upande ,Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Bw. Asangye Bangu,amewapongeza wahitimu hao kwa kumaliza mafunzo hayo huku akiwataka mafunzo waliyoyapata  kuyatumia katika utendaji kazi wao.
“Matarajio yetu  tumekufundisha umeelewa,fanya kazi ukiona kitu cha kibunifu usiache kuwasiliana na wataalamu,usifanye maamuzi mwenyewe wasiliana na sisi.Tusisababishe matatizo kwa tamaa,”amesema
Pia  amesema lengo la mafunzo hayo ni  kuhakikisha watendaji katika maghala wanafuata utaratibu kwa maana ya ubora na uzito.
“Timu za wataalamu zinaendelea kuwapatia mafunzo  mara kwa mara mafanikio ni makubwa sasa hivi tuna mazao 16 tulianza na Mikoa ya  Kusini, leo tupo  zaidi ya mikoa 24 huu ndio mfumo mzuri kwani unaweza  kumsaidia mkulima kupata bei ya ushindani,”amesema Bw.Bangu
Kuhusu ufungaji wa CCTV  kamera katika maghala amesema tayari Serikali
imetoa Sh milioni  126 kwa ajili ya kununua CCTV Camera ambazo zitafungwa katika maghala mbalimbali nchini.
“Tutahakikisha  maghala yote yanakuwa na camera kwa ajili ya kutoa taarifa kwani baada ya kufunga wizi umepungua,”amesema
Mhitimu wa mafunzo hayo, Christina Gerald amesema kupitia mafunzo hayo amejifunza vitu vingi ikiwemo kujua mnyororo wa thamani katika mazao.
MWENYEKITI wa Kamati ya Huduma ya Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,Godwin Mkanwa,akizungumza leo Juni 28,2025 Jijini Dodoma  wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa Stakabadhi Ghala  kuelekea Msimu wa mazao ya Mbaazi na Dengu 2025-2026.

MWENYEKITI wa Kamati ya Huduma ya Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,Godwin Mkanwa,akisisitiza jambo kwa wahitimu wa mafunzo wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa Stakabadhi Ghala  kuelekea Msimu wa mazao ya Mbaazi na Dengu 2025-2026.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Bw. Asangye Bangu,akizungumza wakati wa kuhitimishwa mafunzo ya ya mfumo wa Stakabadhi Ghala  kuelekea Msimu wa mazao ya Mbaazi na Dengu 2025-2026 yaliyomalizika leo Juni 28,2025 jijini Dodoma.
SEHEMU ya wahitimu wa mafunzo wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti  wa Kamati ya Huduma ya Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,Godwin Mkanwa,(hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa Stakabadhi Ghala  kuelekea Msimu wa mazao ya Mbaazi na Dengu 2025-2026.

Mwenyekiti  wa Kamati ya Huduma ya Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,Godwin Mkanwa,akikabidhi vyeti kwa wahitimu mbalimbali wa  mafunzo ya mfumo wa Stakabadhi Ghala  kuelekea Msimu wa mazao ya Mbaazi na Dengu 2025-2026 yaliyomalizika leo Juni 28,2025 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor