Burudani Featured

AGGY BABY ATANGAZA RASMI EP MPYA “FIRST LOVE”

Written by mzalendoeditor
Msanii maarufu wa muziki, mwigizaji, na mwanaharakati wa kijamii kutoka Tanzania, Agness Suleiman, anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii Aggy Baby, amezindua rasmi EP (Album) yake ya kwanza iitwayo “First Love”. EP hii inaonyesha mchanganyiko wa mitindo ya muziki kama Bongo Fleva, Amapiano na Kompa, ikiwakilisha sauti mpya ya muziki wa Afrika Mashariki.
EP “FIRST LOVE ” (2025) Album
EP (Album) hii ina nyimbo sita zinazochanganya hisia, ujasiri na mtazamo mpya wa maisha na mapenzi:
Wanipa – Wimbo wa kwanza unaogusa hisia ya mapenzi ya wapendanao .
Watajuaje – Kibao cha Bongo Flava kinachogusa maisha halisi ya watu na tafsiri ya mapenzi kwa jicho la jamii.
Kamnyweso (feat. Stompion) – Amapiano yenye nguvu, inayowafanya watu wasimame na kucheza.
On The Bed (feat. Mr LG) – Wimbo wa kipekee wa mahaba unaochanganya sauti mbili zenye mvuto wa kipekee.
I Like That (feat. Baddest 47) – Mchanganyiko wa party vibe na ujanja wa kisasa.
Nimekoma – Ujumbe mzito wa kuachana na mahusiano yasiyo na tija, ukiwasilishwa kwa sauti ya maumivu lakini yenye matumaini.
Ametudokeza kuwa Nyimbo zote tayari zimeshafanyia video na mashabiki zake wote wakae mkao wa kula kwani amepanga kuwasuprise kwa mwaka huu
Pia ameingia kwenye Tuzo kubwa za Africa Arts Entertainment Awards 2025 (aaea)
Unaweza kumfuatilia kwenye mitandao yake ya kijamiii kama Instagram : @aggybaby__
Facebook : aggybaby
Youtube : aggybabys

About the author

mzalendoeditor