Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii Dkt. Rashid Mfaume kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI amewataka Watumishi wa Sekta ya afya katika ngazi ya Afya Msingi kuzingatia viwango (SOP) na ubora wa huduma za afya katika utekelezaji wa majukumu yao ya Kila siku.
Dkt. Mfaume amesema hayo katika Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo katika ziara yake ya kikazi inayoendelea mkoani Dar es Salaam yenye lengo la kuangalia upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii.
“wakati tunatoa hamasa Kwa wananchi wanapo kuja katika maeneo yetu kupata huduma lazima na Sisi kama watendaji tuwe mfano Kwa kuishi viwango vya ubora Kwa huduma ili tutoe bora na Salama”.
Amesema Kwa kuzingatia viwango vya utoaji huduma katika maeneo ya kutendea kazi itasidia kumlimda mtoa huduma za afya na kumlimda mteja anayepokea huduma.
Aidha, Dkt. Mfaume amesema pia Watumishi wanaofanyakazi Kwa kukiuka misingi na viwango vya utoaji wa huduma za afya anafanya kosa kisheria kwani viwango hivyo vimekubalika kitaifa na kimataifa kupitia vyama vya taaluma na bodi taaluma zinazowasimamia Watumishi hao.