Featured Kitaifa

NACTVET YAWAKUTANISHA WADAU WA ELIMU DODOMA KUJADILI MABADILIKO YA KANUNI ZA UDAHILI VYUO VYA ELIMU YA KATI

Written by mzalendoeditor

KAIMU  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET),Dkt.Jofrey Oleke,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Warsha ya Wadau kuhusu  kupitia Kanuni za Udahili wa Wanafunzi,Mitihani,Usajili wa Vyuo na Ithibati ya Vyuo vya Elimu ya Kati, iliyofanyika leo Machi 28,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Kaimu   Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET),Dkt.Jofrey Oleke (hayupo pichani) wakati akifungua  Warsha ya Wadau kuhusu  kupitia Kanuni za Udahili wa Wanafunzi,Mitihani,Usajili wa Vyuo na Ithibati ya Vyuo vya Elimu ya Kati, iliyofanyika leo Machi 28,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi  wa Uthibiti Ubora wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Dkt. Jofrey Oleke (hayupo pichani) wakati akifungua  Warsha ya Wadau kuhusu  kupitia Kanuni za Udahili wa Wanafunzi,Mitihani,Usajili wa Vyuo na Ithibati ya Vyuo vya Elimu ya Kati, iliyofanyika leo Machi 28,2025 jijini Dodoma.

Katibu wa Umoja wa Wakuu wa Vyuo Tanzania, Mwl. Rashid Nditi,akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau kuhusu  kupitia Kanuni za Udahili wa Wanafunzi,Mitihani,Usajili wa Vyuo na Ithibati ya Vyuo vya Elimu ya Kati, iliyofanyika leo Machi 28,2025 jijini Dodoma.

Na  Alex Sonna-DODOMA
WADAU wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi  wamekutana Jijini Dodoma kujadiliana kanuni mbalimbali ambazo wanazitumia za usajili wa vyuo,udahili wa wanafunzi katika vyuo vya ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Akizungumza leo Machi 28,2025 jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao hicho,Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTVET,Dkt Jofrey Oleke, amesema lengo la kikao hicho ni  kupata maoni ya wadau kabla kanuni hazijaanza  kutumika.
“Ikumbukwe kwamba zinahuishwa kutokana na mabadiliko mbalimbali katika sera ya elimu na Mafunzo 2014 na toleo la 2023 ambayo imezinduliwa na Rais( Samia Suluhu Hassan)”amesema Dkt.Oleke.
Amesema malengo ya kuhuisha kanuni hizo ni pamoja na kanuni kuendana na sera na mabadiliko ikiwemo kusimamia suala la ubora.
Amesema manufaa makubwa ya kanuni hizo ni pamoja na kupata miongozo bora ambayo itatumika kuhakikisha ubora wa elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi unaongezeka.
“Na zitasaidia kupata wahitimu bora ambao watalisaidia Taifa kwa sababu wanaohitajika wataalamu ambao ni bora katika soko la ajira,”amesema
Kwa upande wake  Katibu wa Umoja wa Wakuu wa Vyuo vya Ufundi Stadi  Tanzania,Mwl Rashid Nditi amesema dhumuni la kikao hicho ni kukumbushana jinsi  ya kufanya usajili wa wanafunzi kwa kufuata maelezo ya NACTVET  
Amesema wamekuwa wakifanya mafunzo hayo mara kwa mara kwani yanawasaidia kufanya kazi kwa  kufuata utaratibu ambao umekuwa ukiwekea  na NACTVET.
Naye,Mkufunzi kutokea Chuo Cha Zimamoto na Ukoani Mkaguzi Msaidizi,Emmy Mwapalolo amesema wapo hapo kwa ajili ya kujadiliana maboresho na mabadiliko ya Sheria mbalimbali.
“Sisi kama wadau tupo mahala hapa kufahamu na kizipitia ili tunapotekeleza majukumu yetu tufuate taratibu,”amesema
Kwa upande wake,Mhitimu wa Chuo Cha Utalii John Kidai,amesema amejifunza maboresho ya sera yatasaidia kupatikana kwa wahitimu bora kwenye soko la ajira.

About the author

mzalendoeditor