Featured Kitaifa

WAZIRI MASAUNI AWAANDALIA FUTARI WABUNGE, AWASHURUKU KWA USHIRIKIANO

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akizungumza wakati wa Iftar aliyowaandalia Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Maji na Mazingira pamoja na Utawala, Katiba na Sheria kushiriki Iftar aliyoandaa jijini Dodoma Machi 24, 2025.

….

Ofisi ya Makamu wa Rais imesema ushirikiano inaoupata katika Kamati za Kudumu za Bunge umekuwa nguzo katika kuimarika kwa Muungano na usimamizi endelevu wa hifadhi ya mazingira nchini.

Hayo yamebainishwa Machi 24, 2025 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni wakati wa IFTAR aliyoiandaa kwa Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Maji na Mazingira pamoja na Utawala, Katiba na Sheria.

Mhe. Masauni amesema katika kipindi cha miaka mitano sasa, kamati hizo  zimekuwa mhimili muhimu katika kusimamia wajibu wake kupitia maelekezo mbalimbali kwa Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika namna bora ya kuimarisha utendaji kazi wenye tija.

“Sote tunatambua namna ya utendaji kazi wetu unavyoimarika, tunazishukuru kamati za Bunge kwa namna zilivyoweza kufanya kazi zake kwa weledi wa hali ya juu na namna inavyopata mrejesho na  ushirikiano kutoka kwa menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais” amesema Waziri Masauni. 

Mhandisi Masauni amesema Ofisi ya Makamu wa Rais inajivunia weledi wa kamati hizo katika kusimamia wajibu wake wa kikatiba ambao umeiwezesha Ofisi ya Makamu wa Rais kushughulikia kwa kasi na mafanikio makubwa hoja za masuala ya Muungano na Mazingira zilizowasilishwa katika vikao vya kamati na mikutano ya Bunge.

Ameeleza kuwa Viongozi, Menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wapo tayari kutoa ushirikiano wowote unaohitajika katika kufanikisha utekelekezaji wa majukumu ya kamati ili kuweza kufikia malengo iliyojiwekea katika kuhudumia wananchi.

“Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kufanya kazi nzuri sana. Nipo Bungeni kwa zaidi ya miaka 15 sasa na moja ya mambo yanayodhihirisha utendaji wa Ofisi hii ni namna wanavyoshughulikia hoja za Muungano ambazo kwa sasa zimebaki hoja 3 kutoka hoja 25 za awali” amesema Mhandisi Masauni.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Mhe. Jackson Kiswaga amesema kamati hiyo itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa majukumu Ofisi ya Makamu wa Rais ili kuleta tija iliyokusudiwa.

“Tumeendelea kulisema hili kila wakati kuwa katika kipindi hiki kifupi, Ofisi hii imeendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa kamati katika kutekeleza majukumu yake……Tunaahidi kufanya kazi muda wote usiku na usiku na mchana ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea” amesema Mhe. Kiswaga.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo amesema Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa Ofisi ya kupigiwa mfano katika Wizara za kisekta katika namna inavyoshirikiana kwa karibu na kamati hiyo katika kutekeleza majukumu na wajibu wa mhimili huo.

“Mmeendelea kuiunganisha vyema kamati na Serikali katika kutekeleza majukumu tuliyonayo, hii ndiyo dhamira ya Viongozi wetu wakuu akiwemo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan” amesema Mhe. Kyombo.

Awali Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja aliwashukuru wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge kwa kutenga muda wao na kujumuika pamoja katika hafla ya Iftar ikizingatiwa wingi wa majukumu waliyonayo katika kipindi hiki ikiwemo maandalizi ya vikao vya mkutano wa Bunge la bajeti.

“Tunawashuru kwa kuweza kujumuika nasi katika Iftar hii ambayo imeandaliwa na Ofisi kwa ajili ya kujumuika pamoja na hii inaonesha ushirikiano mkubwa mnaoendelea kutupatia katika kutekeleleza majukumu yetu” amesema Mhandisi Luhemeja.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akijumuika na Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Maji na Mazingira pamoja na Utawala, Katiba na Sheria kushiriki Iftar aliyoandaa jijini Dodoma Machi 24, 2025. Kushoto ni Katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis na katikati ni Mbunge wa Bukene Mhe. Selemani Zedi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga akishiriki Iftar iliyoandaliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kwa ajili ya kamati hiyo pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma Machi 24, 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akizungumza wakati wa Iftar aliyowaandalia Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Maji na Mazingira pamoja na Utawala, Katiba na Sheria kushiriki Iftar aliyoandaa jijini Dodoma Machi 24, 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (wa pili kulia) akijumuika na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga (wa pili kushoto) na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis kushiriki Iftar aliyoandaa kwa Kamati za Kudumu za Bunge za Maji na Mazingira pamoja na Utawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma Machi 24, 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akiteta jamb na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa Iftar aliyoandaa kwa Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Maji na Mazingira pamoja na Utawala, Katiba na Sheria na Viongozi jijini Dodoma Machi 24, 2025.

Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Maji na Mazingira pamoja na Utawala, Katiba na Sheria na Viongozi na watendaji Ofisi ya Makamu wa Rais wakishiriki Iftar iliyoandaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusuf Masauni jijini Dodoma Machi 24, 2025.

About the author

mzalendoeditor