Na Mwandishi Wetu, Manyara
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe.Mohamed Khamis Hamad ametoa wito kwa wakazi wa Kata ya Babati kutoa taarifa ya matukio ya kikatili pindi yanapotokea katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mjengo Kata ya Babati Machi 20,2025 Mkoani Manyara.
Mhe.Mohamed Hamad amesema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya Jamii kujichukulia sheria mkononi maamuzi ambayo ambayo yanamnyima mtu haki ya kuishi.
Awali akiainisha majukumu ya THBUB, Mhe Mohamed amesema kuwa THBUB imefika katika kata hiyo kwa lengo la kutoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora pamoja na kupokea malalamiko ya wakazi hao yanahusu uvunjifu wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
‘Niwaombe nafasi hii muitumie vizuri kuwasilishe malalamiko yenu ili yapatiwe ufumbuzi.
Upokeaji wa malalamiko kutoka kwa wananchi ni mojawapo wa utekelezaji wa majukumu ya Tume ambayo yameainishwa katika ibara 130 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.