Featured Kitaifa

TBA YAPONGEZWA KWA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI NZUGUNI

Written by mzalendoeditor
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakipata maelezo wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.
Na.Mtemi Sona-Dodoma 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni, jijini Dodoma.
Kamati hiyo imetoa pongezi hizo baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo, ambao kwa sasa uko katika awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba 60 za chinu na nyumba 90 za ghorofa. Tayari nyumba 150  za awamu ya kwanza zimekamilika na zinatumika kwa makazi.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Augustine Vumma (Mb), amesema mradi huo umebuniwa kwa ubunifu wa hali ya juu na unatekelezwa kwa viwango vinavyoridhisha. Amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha nyumba hizo zinatunzwa vizuri ili zidumu kwa muda mrefu.
“Tumeona kazi nzuri iliyofanyika, ni mradi mzuri unaovutia. Tunashauri TBA kushirikiana na taasisi kama TARURA ili kuboresha miundombinu ya barabara ndani ya mradi huu kwa kiwango cha lami,” amesema Mhe. Vumma.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kondoro, amesema TBA itaingia ubia na sekta binafsi ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa haraka na kwa ufanisi. Amebainisha kuwa TBA tayari imesaini makubaliano na wawekezaji kutoka nje ambao watashiriki katika awamu ya pili ya mradi.
“Mbali na kushirikiana na sekta binafsi, tunapunguza gharama za ujenzi kwa kuwa na kiwanda cha kuchakata zege hapa Nzuguni,” amesema Arch. Kondoro.
Mradi huo unatekelezwa kwa awamu na utakapokamilika utajumuisha huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo shule, zahanati, maeneo ya kucheza na maeneo ya kupumzika.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakikagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakipata maelezo wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakipata maelezo wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),wakipata maelezo wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma,ziara iliyofanyika leo Machi 12,2025.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),Mhe.Augustine Vuma,akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 12,2025 mara baada ya kamati yake kufanya  ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na Umeme(DTES), Mhandisi Mwanahamisi Kitogo,akiipongeza Kamati  ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kwa kufanya  ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kondoro,akitoa maelezo kwa Kamati  ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor