Uncategorized

JK ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA KIBINGWA ZA MATIBABU ZINAZOTOLEWA NA BMH

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameridhishwa na hatua za utekelezaji wa maono aliyokuwa nayo wakati akianzisha Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya kuifanya kuwa kituo cha umahiri cha matibabu ya figo, pamoja na huduma zingine za ubingwa wa juu.

Rais mstaafu, Kikwete, ameyasema hayo leo alipotembelea BMH jijini Dodoma, huku akibainisha kuwa kipindi cha nyuma watanzania walikuwa wanapata shida ya huduma za matibabu ya figo ikiwemo huduma ya uchujaji wa damu (dialysis) na hivyo kulazimika kuzifuata Nairobi Kenya.

“Vision yangu wakati tunaanzisha BMH ilikuwa kuanzisha Hospitali ambayo itakuwa kutuo cha umahiri nchini katika matibabu ya figo, na huduma zingine za ubingwa wa juu. Nimefurahi ndoto yangu imetimia na sasa BMH inatoa huduma za kibingwa za Matibabu ya figo ikiwemo uchujaji wa damu, upandikizaji figo, lakini pamoja na hatua hiyo kubwa ambayo imefikiwa, haizuii BMH kuwekeza katika utoaji huduma za matibabu ya magonjwa mengine,”  amesema Rais mstaafu wakati ya ziara yake BMH.

Rais mstaafu ametembelea huduma mbalimbali za BMH ikiwemo upandikizaji uloto, huduma ya matibabu ya figo, matibabu ya moyo na jengo linalojengwa la matibabu ya saratani.

Mhe. Kikwete pia amefurahishwa na Serikali kuendeleza huduma za Tiba ya figo na kupanua zingine ndani ya Hospitali ya Benjamin Mkapa.

“Hii ni five star hospital, tulipanga pamoja na kwamba tulipanga iwe Centre of Excellence ya matibabu ya figo lakini tulitaka itoe matibabu mengine ya ubingwa wa juu na imesadifu hayo maono,” amesema Mhe. Kikwete. Mheshimiwa Rais mstaafu amefarijika pia na kuona huduma za hali juu katika uchunguzi na tiba ya Moyo, pamoja na Upandikizaji Uloto.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Prof Abel Makubi, amesema mpaka sasa BMH imefikisha watu 50 waliopandikizwa figo toka huduma ilipoanza.”Tumeokoa 1.6 bn/- ambazo zingetumika kuwapa rufaa watanzania nje ya nchi kwa ajili ya upandikizaji wa figo,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa BMH.

Kuhusu jengo jipya la huduma za matibabu ya Saratani, Prof Makubi, amesema ujenzi wa jengo umefikia.

About the author

mzalendo