Burudani Featured

Wimbo Mpya : AGNESS SULEIMAN Ft. CRIMMY – NIMEKOMA

Written by mzalendoeditor

Mwanamuziki na Muigizaji maarufu nchini  Tanzania Agness Suleiman 18 Oktoba  ameachia rasmi wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la ‘NIMEKOMA’ wenye uhalisia wa zouk (kompa)

Kwa mujibu wa Agness Suleiman amesema tayari wimbo huo ambao amemshirikisha  Crimmy unapatikana kwenye ‘platform’ zote za muziki za mitandaoni ikiwemo Boomplay, Youtube,  iTunes,  Audiomack na zingine nyingi.

Agness pia bado yupo kwenye chati kubwa za muziki akitamba na wimbo wake wa ‘WANIPA’.

Agness  mbali ya kuimba pia ni ,msanii wa filamu (Actress ), mtunzi na Mwandishi wa nyimbo na Mwanaharakati wa Vijana katika mambo ya kusaidia jamii kupitia taasisi yake ya Tupaze Sauti Foundation 

Wimbo huo wa ‘NIMEKOMA’ pia unaweza kuupata kupitia link hii https://youtu.be/hiSkwwXUWXc?si=5JlD2gQH6Dx2oOC3 na kufuatilia kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kama facebook, twitter,linkedln na instagram kwa jina la Agness suleiman.

About the author

mzalendoeditor