Featured Kitaifa

MAWAZIRI WAWEKA MIKAKATI KULINDA ZIWA TANGANYIKA

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza wakati wa Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Nchi za Ziwa Tanganyika zinazoundwa na Tanzania, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa kujadili kuongezeka kwa kina cha ziwa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 04, 2024.

Mwenyekiti wake Mawaziri wa Nchi za Ziwa Tanganyika ambaye pia ni Waziri wa Uchumi wa Kijani na Mazingira Mhe. Mike Mpasho (wa pili kushoto) akiwa pamoja na viongozi wengine kuanzia kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis, Waziri wa Uvuvi na Mifugo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Jean Pierre Tshimanga na Katibu Mkuu Wizara ya Mazingira, Kilimo na Uvuvi ya Burundi Bw. Emmanuel Ndorimana

Washiriki kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Nchi za Ziwa Tanganyika zinazoundwa na Tanzania, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa kujadili kuongezeka kwa kina cha ziwa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 04, 2024.

Mawaziri wa Nchi za Ziwa Tanganyika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Nchi za Ziwa Tanganyika zinazoundwa na Tanzania, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa kujadili kuongezeka kwa kina cha ziwa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Serikali ya Tanzania imesema Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ametoa wito kwa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika kuendelea kulinda ziwa hili ili lisaidie katika shughuli za kijamii.

Ametoa wito huo wakati akizungumza wakati wa Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika zinazoundwa na Tanzania, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wa kujadili kuongezeka kwa kina cha ziwa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mhe. Khamis amesema kuwa pamoja na changamoto hizo, zipo hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania inachukua ili kuhakikisha Ziwa Tanganyika linakuwa salama kimazingira.

Amesema Serikali imekuwa ikihimiza wananchi hususan wale wanaozunguka ziwa hilo kupanda miti katika maeneo yanayolizunguka ili kupunguza kutokea kwa mmomonyoko wa udongo na kuathiri bonde la ziwa.

Halikadhalika, Naibu Waziri Khamis amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya uvuvi usio endelevu na zisizo rasmi ambazo kwa kiwango kikubwa zinachangia katika uharibifu wa mazingira.

“Kama nchi tunasimamia Sheria za Uvuvi ili wananchi wetu waweze kuzifuata ili lengo la kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi litimie na hatimaye maji haya ya ziwa yawe yanapungua siku hadi siku,“ amesisitiza.

Katika hatua nyingine, nchi nne zinazozunguka Ziwa Tanganyika zimekubaliana kulinda ziwa hil kwa kuanzisha mfumo wa taarifa za hali ya hewa na tahadhari za mapema ili kuimarisha mbinu za kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wake Mhe. Mike Mposha amesema nchi hizo pia zimeweka mpango imara wa hali ya dharura na maafa kwa wananchi waishio katika bonde la ziwa hilo.

Mhe. Mposha ambaye pia ni Waziri wa Uchumi wa Kijani na Mazingira

alisema umefika wakati wa kutekeleza mipango ya kurejesha maeneo yaliyoharibika na kuhakikisha kuwa hifadhi ya mazingira ya bonde inakuwa endelevu na kuwanufaisha wananchi hao.

Aidha, amekumbusha kuwa Bonde la Ziwa Tanganyika bado lina changamoto ya kungezeka kwa kina cha maji, mabadiliko ya tabianchi uharibifu wa misitu na ikolojia, hivyo ni wajibu wa mataifa hayo kushirikiana na kukabiliana nazo.

“Utekelezaji wa maazimio ambayo mkutano huu umepitisha yapewe kipaumbele na nchi wanachama, Mamlaka ya Ziwa Tanganyika (LTA) na washirika wetu ili kushughulikia changamoto,” amesisitiza Mhe. Mpasho.

Pamoja na hayo pia, Waziri Mpasho ameipongeza Serikali ya Tanzania ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo kwa juhudi za kuhakikisha Ziwa Tanganyika na Bonde lake kwa ujumla linalindwa.

Nchi Wanachama zinazozunguka Ziwa Tanganyika ni Tanzania ambayo katika mkutano huo iliwakilishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis, Zambia (Mhe. Mposha), Waziri wa Uvuvi na Mifugo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Jean Pierre Tshimanga na Katibu Mkuu Wizara ya Mazingira, Kilimo na Uvuvi Bw. Emmanuel Ndorimana.

Awali, kabla ya mkutano huu wataalamu na baadae menejimenti ya LTA walikutana kujadili utatuzi wa changamto ya kuongezeka kwa kina cha maji ya Ziwa Tanganyika jijini Dar es Salaam

 

About the author

mzalendoeditor