Featured Kitaifa

NCHIMBI: CHANGAMOTO ZA BODABODA, MACHINGA ZISHUGHULIKIWE

Written by mzalendo

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dokta EMMANUEL NCHIMBI, ameipongeza Serikali ya Mkoa wa Geita, kwa kuchukua hatua mbalimbali za kushughulikia changamoto zinazowakabili Bodaboda na Wamachinga mkoani Geita.

Changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa matukio ya kutekwa kwa Bodaboda na Pikipiki zao na kutokamilika kwa ofisi za Bodaboda na Wamachinga.

Balozi Dokta NCHIMBI amesema hayo alipokua akizungumzia kero za Bodaboda ikiwemo kuwepo kwa matukio ya kutekwa kwa Bodaboda na Pikipiki zao, na pia changamoto ya kutokamilika kwa Ofisi ya Bodaboda na Machinga mkoani Geita.

Amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani Geita katika uwanja wa Shule ya msingi Uwanja ikiwa ni muendelezo wa ziara yake Kanda ya Ziwa.

Akijibu kero hizo Mkuu wa Mkoa wa Geita MARTINE SHIGELA amesema Serikali mkoa wa Geita, tayari imetekeleza maagizo ya Rais Dokta SAMIA SULUHU HASSAN ya kuwajengea Ofisi Machinga, ambapo tayari Rais Dokta SAMIA alitoa Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya kuanza safari ya Ujenzi huo.

RC SHIGELA amesema tayari wamejenga na Ramani waliyopewa, waliipanua iwe kubwa zaidi, na wanatarajia mpaka tarehe 15 mwezi wa 9, kutakua na sherehe ya kuwakabidhi Ofisi Machinga na Bodaboda.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Balozi Dokta NCHIMBI, ametaka Serikali mkoa wa Geita kuongeza kasi ya kuinua wachimbaji wadogo na Wafanyabiashara wadogo mkoani humo.

Amesema hayo alipokua akizungumzia kuhusu taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Geita MARTINE SHIGELA inayoonesha wachimbaji wadogo zaidi ya elimu mbili walipata Leseni.

About the author

mzalendo