Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, leo ametembelea Maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane jijini Dodoma ambapo alipata wasaa wa kutembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.
Akipokewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, Dkt. Kusiluka alipata fursa ya kuungana na wananchi mbalimbali kutembelea Banda hilo na kujionea wanyama mbalimbali wakiwemo Simba, Chui, Pundamilia, Nyumbu, Fisi na jamii mbalimbali za ndege.
“Mpaka kufikia jana watu zaidi ya 17,000 walikuwa wamepata fursa hii ya Nane Nane kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea wanyama katika eneo hili,” alieleza Dkt. Abbasi.
Kwa upande wake Dkt. Kusiluka amepongeza ubunifu wa Wizara hiyo katika kuhakikisha wanatumia maonesho hayo kutangaza utalii.