Featured Kitaifa

RC RUVUMA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA 50 YENYE THAMANI YA BIL. 14

Written by mzalendo

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed A. Ahmed leo tarehe 6 Agosti,2024 ameshuhudia utiaji saini wa mikataba 50 yenye thamani ya shilingi bilioni 14 baina ya TARURA na Wakandarasi kwaajili ya matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa mkoa wa Ruvuma kwa mwaka 2024/2025.

About the author

mzalendo