Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Gates Foundation Bw. Mark Suzman yaliyofanyika kwa njia ya mtandao (Video Call) tarehe 10 Julai, 2024. Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Taasisi hiyo na kujadili maeneo mengine ya ushirikiano ikiwemo katika masuala ya afya, kilimo, uwezeshwaji wanawake kiuchumi, uchumi jumuishi, Elimu na matumizi ya akili bandia (AI) katika maeneo tajwa.