KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali ameiagiza Tume ya Madini chini ya Katibu Mtendaji wake, Mhandisi Yahya Samamba kuongeza kasi ya kutatua migogoro ya wachimbaji wa madini nchini.
Mahimbali ametoa maelekezo hayo leo Juni 27, 2024 alipotembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Convention Centre (JKCC) jijini Dodoma.
Amesema, Tume inafanya kazi nzuri ya kukusanya maduhuli, mapato yameongezeka na yanaonekana na kuitaka iongeze kasi ya kutatua changamoto za wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwa wanachangia asilimia 40 ya mapato katika Sekta ya Madini
” Msi -ignore wachimbaji wadogo, STAMICO hata kama ni walezi na nyie Tume mna ‘role’ yenu, ” amesema Mahimbali.