Featured Kitaifa

WAZIRI JAFO: ASILIMIA 79.3 YA MITI ILIYOPANDWA IMESTAWI

Written by mzalendo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijibu maswali bungeni wakati wa Kikao cha 44 Mkutano wa 15 wa Bunge jijini Dodoma leo Juni 10, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni wakati wa Kikao cha 44 Mkutano wa 15 wa Bunge jijini Dodoma leo Juni 10, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiteta jambo na Naibu Waziri wake, Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati wa Kikao cha 44 Mkutano wa 15 wa Bunge jijini Dodoma leo Juni 10, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akishiriki Kikao cha 44 Mkutano wa 15 wa Bunge jijini Dodoma leo Juni 10, 2024. Katikati ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis

jibu maswali bungeni wakati wa Kikao cha 44 Mkutano wa 15 wa Bunge jijini Dodoma leo Juni 10, 2024.

……

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema hadi kufikia Machi 2024 miti milioni 266 imepandwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara.

Dkt. Jafo amesema hayo wakati akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Juni 10, 2024 ambapo amebainisha kati ya hiyo, miti milioni 211 imekukua, ambayo ni sawa na asilimia 79.3.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mhe. Aida Khenan aliyeuliza kuhusu utoaji wa taarifa ya mazoezi ya upandaji wa miti, Dkt. Jafo amesema Ilani ya Uchaguzi imeelekeza kila halmashauri nchini kupanda miti milioni 1.5 hivyo, takwimu hizo zinaonesha namna Serikali inavyoendelea na utekelezaji wake.

Awali, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Serikali imetunga na inasimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo ili kuzuia ukataji holela wa miti katika maeneo ya milimani na miinuko

Amesema hayo wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kalenga aliyeuliza ni lini Serikali itatunga sheria kali ya kuzuia ukataji miti holela hasa kwenye maeneo yenye milima na miinuko ili kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Naibu Waziri Khamis ametaja Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Mazingira Sura 191, Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 na Sheria ya Misitu Sura 323 ambazo zina vifungu mahususi kuhusu hifadhi ya mazingira na Ulinzi wa milima, vilima na miinuko. 

Amesema sanjari na kutunga sheria, Serikali imechukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha mazingira ya nchi yanalindwa na kuhifadhiwa vizuri zikiwemo kuandaa na kutekeleza Mkakati wa Hatua za Haraka Kuhifadhi Mazingira ya Ardhi na Vyanzo vya Maji wa mwaka 2006 unaoweka lengo la kila wilaya kupanda miti milioni 1.5) kila mwaka na Mkakati wa Taifa wa Kupanda na Kutunza Miti wa miaka mitano (2016/17 – 2020/2021). 

Ameongeza kuwa ili kuongeza jitihada za uhifadhi katika maeneo ya milima na miinuko, Ofisi ya Makamu wa Rais itashirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mamlaka za Serikali za Mtaa na Sekta Binafsi katika kutoa elimu na kusimamia sheria zilizopo kwa sasa.

aelezo ya Ziada 

Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura 191 Kifungu cha 58(2) kinaelekeza kuhusu hifadhi ya mazingira na Ulinzi wa milima, vilima na miinuko; na Sera ya Misitu ya mwaka 1998 imeelekeza utaratibu wa kutunza na kuhifadhi milima na miinuko. Aidha, Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999; na Sheria ya Misitu Sura 323, zimeweka utaratibu wa kisheria wa kudhibiti uharibifu wa mazingira hususan ukataji miti holela katika maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya milima na miinuko.

Maelezo ya Ziada 

Katika hatua nyingine akijibu swali la Mhe. Khamis amepiga marufuku shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji ndani ya mita 60 na miinuko na kuelekeza upandaji wa miti ya kutosha kwatika maeneo hayo. 

Amesema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mhe. Kiswaga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira aliyeuliza mpango wa Serikali wa kutoa tamko la zuio la kufanya shughuli za kibinadamu kwenye miinuko.

Itakumbukwa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura 191 Kifungu cha 58 (2) kinaelekeza kuhusu hifadhi ya mazingira na ulinzi wa milima, vilima na miinuko na Sera ya Misitu ya mwaka 1998 imeelekeza utaratibu wa kutunza na kuhifadhi milima na miinuko. 

Halikadhalika, Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 na Sheria ya Misitu Sura 323, zimeweka utaratibu wa kisheria wa kudhibiti uharibifu wa mazingira hususan ukataji miti holela katika maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya milima na miinuko.

About the author

mzalendo