Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameshiriki katika Kikao cha Baraza la Mawaziri wa Kisekta kwa ajili ya Maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Waziri wa Nchi katika Ofisi hiyo Mhe. Jenista Mhagama kuhusu Hali ya Mvua za El Nino utakaofanyika kwa njia ya Mtandao (Zoom meeting) leo tarehe 20 Mei 2024.
Kikao hicho kimefanyika katika UKumbi wa Ofisi hiyo kwa njia ya mtandao tarehe 19 Mei 2024 Jijini Dodoma.