Featured Kitaifa

MILIONI 300 KUKAMILISHA UJENZI JENGO LA KUHIFADHIA MAITI HOSPILI YA RUFAA MKOA WA KATAVI

Written by mzalendoeditor

Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la kuhifadhia Maiti Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi.

Kauli hiyo imebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 254 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Taska Restituta Mbogo aliyeuliza Je, lini Serikali itajenga jengo la kuhifadhia Maiti Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi.

Dkt. Mollel amesema ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi utaanza kutekelezwa kabla ya mwaka wa fedha 2023/2024 kuisha na kukamilishwa mwaka wa fedha 2024/2025.

“Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024 Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 12.9 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi”, ameeleza Dkt. Mollel.

Dkt. Mollel ameongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake amegawa magari ya kubebea wagonjwa katika halmashauri zote nchini hivyo na hivi karibuni Mkoa wa Katavi wataongezewa gari la kubea wagonjwa.

About the author

mzalendoeditor