Featured Kitaifa

EWURA  YATOA VIBALI SITA KWA AJILI YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA KUSAMBAZA GESI ASILIA

Written by mzalendo

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko  akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2024/25 leo Aprili 24,2024 bungeni jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

HADI kufikia Machi 2024 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilitoa vibali sita kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ya kusambaza gesi asilia viwandani na vituo vya kujazia gesi kwenye magari (CNG).

Hayo yamesemwa leo Aprili 24,2024 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2024/25.

Dkt.Biteko amesema kuwa vibali hivyo vilitolewa kwa TPDC  kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikuu cha kuzalisha CNG kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Vituo vidogo viwili vya kupokea CNG katika kiwanda cha Kairuki (Kibaha) na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Vibali vingine viwili kwa ajili ya ujenzi wa mabomba ya kuunganisha gesi asilia kwenye kituo cha kujazia gesi kwenye magari ya Dangote na kwenye kiwanda cha Kampuni ya KEDA vilivyopo Mkuranga.”amesema

Aidha amesema kuwa EWURA ilitoa kibali cha ujenzi kwa Kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania (PAET) kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi la kuunganisha kituo cha kujazia gesi asilia kwenye Magari cha Kampuni ya TAQA Dalbit-Kipawa.

Pia EWURA ilitoaa leseni mbili za uendeshaji kwa vituo viwili vya kujazia gesi asilia kwenye Magari.Vituo hivyo vinamilikiwa na Kampuni za TAQA Dalbit (Kipawa-Dar es Salaam) na Dangote (Mkuranga-Pwani) vinavyohudumia watumiaji wa Nishati ya gesi asilia kwenye maeneo husika.

About the author

mzalendo