Featured Kitaifa

WAAJIRI WOTE NCHINI WATAKIWA KUSAJILI MAENEO YAO YA KAZI OSHA

Written by mzalendo
WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi ,Vijana ,Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Mhe.Deogratius Ndejembi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Duniani inayofanyika ,Aprili 28,2024  jijini Arusha.

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi ,Vijana ,Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Mhe.Deogratius Ndejembi,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Duniani inayofanyika ,Aprili 28,2024  jijini Arusha.

WAANDISHI wa Habari wakimsikiliza Waziri   wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( kazi ,Vijana ,Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Mhe.Deogratius Ndejembi,akizungumza  kuhusu Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Duniani inayofanyika ,Aprili 28,2024  jijini Arusha.

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi ,Vijana ,Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Mhe.Deogratius Ndejembi,akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda wakati akizungumza na  waandishi wa habari kuhusu Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Duniani inayofanyika ,Aprili 28,2024  jijini Arusha.

Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( kazi ,Vijana ,ajira na Watu wenye ulemavu) Mhe.Deogratius Ndejembi amewataka waajiri wote nchini  kuhakikisha  wanasajili maeneo yao ya kazi OSHA pamoja na kuendelea kutekeleza taratibu mbali mbali za usalama na afya kwa mujibu wa Sheria.
Ndejembi ametoa kauli hiyo leo Aprili 22,2024 jijini Dodoma ,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea ,Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya  mahala pa kazi Duniani iyofanyika tarehe 28 Aprili 2024 jijini Arusha.
Amesema kuwa Serikali ,inatambua umuhimu wa kulinda NguvuKazi ya Taifa.
  “Kupitia Taasisi ya OSHA, Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 miongoni mwa wadau na Watanzania wote kwa ujumla.”amesema Waziri Ndejembi
 Waziri Ndejembi amesema  lengo ni kuhakikisha kwamba maeneo yote ya kazi nchini yanakuwa na mifumo madhubuti ya kuwakinga wafanyakazi dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

” Serikali kwa kushirikiana na wadau wetu wa Utatu tunaendesha kampeni maalum ya uhamasishaji kupitia shughuli za mafunzo ya Usalama na Afya miongoni mwa makundi mbali mbali wakiwemo wajasiriamali wadogo na watu wenye ulemavu”amesema

Aidha amesema kuwa katika Maonesho hayo yatawakutanisha wamiliki/wasimamizi wa sehemu za kazi na wadau wengine ili kutoa elimu kwa umma na kubadilishana uzoefu miongoni mwao juu ya masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi.

Hata hivyo ametoa wito kwa wamiliki wa sehemu za kazi, waajiri, wafanyakazi, na wananchi wote kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika shughuli zote zinazohusu maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi.

“Ninawasihi wananchi wote hasa Wananchi wa Mkoa wa Arusha ili waweze kutembelea maonesho yatakayoanza tarehe 23 hadi 30 Aprili 2024 ambapo tutajumuika pamoja kutafakari hali ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi hapa nchini kwetu.”amesisitiza

Amesema Takwimu za kidunia zilizotolewa na Shirika la Kazi Duniani mwaka 2022 zinaonesha kwamba zaidi ya watu milioni 2.9 hupoteza maisha kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

“Zaidi ya wafanyakazi milioni 402 huumia wakiwa kazini na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa kipindi chote wanachopatiwa matibabu hadi hapo watakapopona.”

Aidha amesema kuwa kwa upande wa  Tanzania jumla ya ajali na magonjwa yaliyoripotiwa katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kuanzia Julai 2019 hadi Juni 2021 ni ajali 4,993 na magonjwa 249. Katika ajali hizo, vifo vilikuwa 217.

Maonesho hayo yatakayofanyika katika Viwanja vya General Tyre jijini Arusha

About the author

mzalendo