Mkuu wa ulinzi wa raia Jamhuri ya Afrika ya Kati Thomas Djimasse amesema takriban watu 58 waliokuwa wakienda kwenye mazishini wamepoteza maisha baada ya boti yao kupinduka majini katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.
Amesema waliweza kutoa miili 58 kutoka mtoni hata hivyo hawajui idadi ya watu ambao wako chini ya maji ameongeza kuwa Watu walioshuhudia boti hiyo ikizama huko Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na picha za video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha kuwa boti hiyo iliyozama ilikuwa imepakia watu zaidi ya 300 wengine wakiwa wamesimama na wengine wamesongamana ndani ya boti hiyo Walikuwa wakielekea katika mazishi ya mkuu wa kijiji wakati ilipopinduka katika Mto Mpoko.
Maurice Kapenya ambaye alikuwa akiisindikiza boti hiyo kwa mtumbwi baada ya kukosa nafasi katika boti hiyo amesema kuwa aliikusanya miili ya baadhi ya wahanga akiwemo dada yake kwa kusaidiwa na wavuvi na wenyeji.
Familia mbalimbali jana zilionekana zikiwatafuta wapendwa wao ambao wanaaminika kuwa wako ndani ya maji huku Majeruhi wa ajali hiyo ya kuzama boti waliookolewa wakiwa wamelekwa hospitali wakiendelea kupata matibabu.
Kujaza watu kupindukia imetajwa kuwa sababu ya ajali hiyo ya boti.