Featured Kitaifa

UVCCM ZANZIBAR WAJIPANGA NA MAPOKEZI YA KISHINDO KWA JOKATE NA ABDI.

Written by mzalendoeditor

Na, Mwandishi wetu Zanzibar..

Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa wametangaza Mapokezi Makubwa na ya Kihistoria ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Ndugu Jokate Urban Mwegelo (MNEC)na Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Ndugu Abdi Mahmood Abdi, Mapokezi hayo yatafanyika siku ya Jumamosi tarehe 20 April 2024 ofisi kuu Zanzibar kuanzia saa 2:00 Asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ofisi kuu ya vijana wa umoja wa CCM Zanzibar,Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujamaaishaji na Chipukizi UVCCM Taifa,Bulugu Magege,amesema wamejipanga vyema kwaajili ya mapokezi ya Heshima ya viongozi hao ambao wameteuliwa hivi karibuni.

“Tarehe 20 Aprili, 2024 Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunatarajia kuwa na mapokezi makubwa na ya kihistoria kwa viongozi wetu ambayo yatafanyika ofisi kuu za UVCCM Zanzibar. Hii ni siku muhimu sana kwa wanachama na wananchi wote waliopo Zanzibar na walio tayari kuja Zanzibar kwa ajili ya tukio hili”.Bulugu Magege Kaimu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa.

“Tunatoa wito kwa wanachama wote na wananchi kwa ujumla kushiriki mapokezi haya kama sehemu ya kuunga mkono viongozi wetu hawa ambao ni hodari na wana uwezo na ueledi mkubwa sana wa kifikra na kiutendaji”. Ndugu Bulugu Magege KMM-Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa.

About the author

mzalendoeditor