Featured Kitaifa

MTATURU:IKUNGI TUNASIMAMA NA SAMIA

Written by mzalendoeditor

 

MBUNGE wa Singida Mashariki Mhe.Miraji Mtaturu,akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),bungeni Jijini Dodoma.

Na.Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Singida Mashariki,Miraji Mtaturu amesema kutokana na kazi nzuri anayoifanya Rais Samia Suluhu Hassan jimboni kwake 2025 wakazi wa Ikungi wanasimama na Rais Samia mpaka kieleweke.

Akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),April 18,2024,Bungeni,Mtaturu amesema mwaka wa fedha wa 2023/2024,Wilaya ya Ikungi imepokea takribani Bilioni 15.

“Ndio maana tunasema hatuna sababu ya kuelekezwa,tunasimama na Rais Samia mpaka kieleweke kuhakikisha kwamba tunampa kura za kutosha, wapiga kelele hawana nafasi tena kwa kuwa vitendo vinaongea kuliko maneno.”amesema.

Amesema katika jimbo la Singida Mashariki jambo hilo halijapata kutokea.

“Sisi tunaposema tunamshukuru Rais tunasema kwa vitendo kwa maana tunayaona, hatukuwahi kuzidi bilioni 3 huko nyuma, leo tunapata bilioni 15 kwetu ni jambo kubwa haijapata kutokea,”

Amesema wamejengewa madarasa 128 mapya katika shule za msingi, madarasa 20 katika shule za Sekondari na kujengewa shule mpya mbili ambapo fedha nyingi zimetumika kwa kazi hiyo.

“Hatukuwa na jengo lolote kutoka ardhi hadi majengo leo hatuwezi kuacha kumsemea Rais kwa kazi anazotufanyia leo watoto wanaenda umbali mfupi kufata masomo kitu ambacho ndio lengo kuhakikisha watoto wanapata elimu bora,”amesema.

Aidha amesema kiasi cha sh. milioni 590 kimetumika kujenga shule mpya ambayo imekuwa kama chuo jambo ambalo ni lazima kumshukuru Rais.

“Kwa sababu miradi ni mingi ninaamini kabisa kwenye eneo la barabara tulikuwa hatuna lami sasa ipo mjini na juzi tumepata tena kilomita moja mkandarasi yupo kazini anaendelea na kazi.”

Upande wa taa za barabarani zimewekwa hivyo Wilaya ya Ikungi ina alama kwa sababu ya namna ambavyo Rais amemua kutekeleza miradi.

“Nampongeza Rais kwa kazi kubwa anayofanya ikiwemo kutoa maelekezo mbalimbali ya kuhakikisha kwamba fedha zinakwenda kwenye miradi ya maendeleo ambayo ipo katika maeneo ya wabunge nchini,”amesema.

Amesema kwa hakika Rais Samia amefanya kazi kubwa katika wizara nyingi na kupeleka fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji majukumu kwa wizara hizo.

“Kwenye vitabu vya dini wanasema moyo usiokuwa na shukrani hukausha mema yote, lakini kushukuru ni kupata thawabu kwa sababu unatambua juhudi ya mwenzako, hivyo kushukuru ni uungwana,”amesema.

USHAURI.

Mtaturu ameshauri kuwa kwa kuwa rasilimali watu ni nyenzo muhimu katika kazi ikiwemo ya kutosha itasukuma juhudi za maendeleo.

Amesema katika halmashauri ya Ikungi wanahitaji watumishi 4,664 lakini wanao 2,369 hivyo upungufu ni watumishi 2,292, sawa na asilimia 50.

“Maana yake kuna watumishi wachache wanabeba mzigo kwa ajili ya wengine hivyo kama tunataka kupata maendeleo ya haraka kule vijijini, mitaani tuongeze watumishi.

Rais Samia ametoa vibali vingi vya utumishi nina amini kwamba tukipata watumishi tunakuwa na mgawanyo kwenye halmashauri zetu, naomba Ikungi tuongezewe ili fedha zinazokwenda kule zisimamiwe vizuri,”ameongeza.

Ametolea mfano eneo la idara ya sheria wanahitajika watumishi wanne hata hivyo aliyepo ni mmoja hivyo kushauri eneo hilo liangaliwe kwa jicho lingine.

PONGEZI KWA TAMISEMI.

Wizara ya Tamisemi ndio ya vijiji, vitongoji na mitaa yote nchini hivyoni kubwa na inagusa maisha ya wananchi wa ndani vijijini hivyo ina umuhimu sana.

“Wilaya ya Ikungi katika jimbo la Singida Mashariki ni mashahidi na nitasema hapa, Nampongeza Mchengerwa kwa kazi nzuri anayofanya kwenye maeneo yetu, hata ya mafuriko yaliyotokea Rufiji naomba Mungu yapite salama ili uweze kurudi mwaka 2020/2025 kwa sababu unamsaidia Rais katika mambo mbalimbali,”amesema.

Amesema kwa hakika kauli ya kusema watu wenye akili huwa wanapigwa vita kwenye maeneo yao imeungwa mkono na watu kwakuwa ameonyesha uwajibikaji wa vitendo.

Mbali na pongezi hizo ameomba Tamisemi impe kiasi cha Sh. Bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa madaraja na barabara ili zipitike wakati wa kwenda kumuombea kura Rais Dkt. Samia.

Amesema ili kukamilisha wizara ya Tamisemi ni lazima kutaja wakuu wa mikoa , wilaya na wakurugenzi ambao wamekuwa wakisimamia maagizo yanayotolewa na Rais na mawaziri.

“Nampongeza Rais kwa kutuletea mkuu wa Mkoa Halima Dendegu mlezi wa wana hakika mama yule tangu amefika ametuunganisha wana Singida kwa pamoja na tumekaa nae na kuzungumza mambo ya maendeleo kwa wananchi wa mkoa huo.”

“Nampongeza Mkuu wa wilaya Thomas Apson, Mkurugenzi Justice Kijazi kwa kazi nzuri wanazofanya ndio maana mnaona Ikungi ya leo sio ya jana kwa sababu fedha zikija zinapelekwa zilipolengwa na maendeleo yanaonekana na wananchi wanashukuru sana,”amesema.

About the author

mzalendoeditor