Featured Kitaifa

EWURA YATAMBULISHA MFUMO WA MAJIS ULIOBORESHWA

Written by mzalendoeditor

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha.Poline Msuya akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Mamlaka za maji kuhusu mfumo wa kieletroni wa MajIs ulioboreshwa kwa ajili ya kupokea taarifa za utendaji wa sekta ya maji, kilichofanyika  EWURA Makao Makuu, Dodoma.

 

Na.Mwandishi Wetu_DODOMA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imefanya kikaokazi cha kutambulisha mfumo wa Majis ulioboreshwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira. Kikao hicho kimefanyia EWURA makao makuu Dodoma.

Akifungua kikao hicho kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Poline Msuya amesema Maboresho yaliyofanyika katika mfumo yalichagizwa pia na maoni ya wadau ambao ni watumiaji wa mfumo. Pia mfumo umeboreshwa kuakisi mabadiliko na maendeleo kwenye sekta ya maji.

Aidha EWURA haitosita kuchukua hatua za kiutawala kwa mamlaka za maji ambazo hazitatekeleza uwasilishaji wa taarifa zao kwa wakati, aliongezea Mha. Poline Msuya.

Akitoa maoni yake muwakilishi wa Wizara ya Maji Mha. Epimack Oscar alisisitiza Mamlaka za Maji zitumie mfumo huo kwa ajili ya kuwa na takwimu sahihi.

Kifungu cha 29(1)(h) cha Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira Sura Namba 272 kinaitaka EWURA kukusanya taarifa za utendaji kutoka mamlaka.

Meneja wa EWURA kanda ya Magharibi Mha. Walter Christopher akiwasilisha mada kuhusu mfumo wa Majis ulioboreshwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwenye kikaokazi cha kutambulisha mfumo huo. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano EWURA makao makuu Dodoma.

Mhandisi Mwandamizi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA, Teophil Sanjawa akiwaelekeza washiriki wa kikaokazi namna ya kujaza taarifa kwenye mfumo wa MajIs ulioboreshwa, leo 17.4.24

Washiriki wa kikao kazi wakifuatilia kwa umakini namna ya kujaza taarifa za utendaji wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira kwenye mfumo wa MajIs ulioboreshwa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Poline Msuya(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za maji za makao makuu ya mikoa na miradi ya kitaifa,wawakilishi kutoka Wizara ya maji na wafanyakazi wa EWURA idara ya Maji muda mfupi baada ya ufunguzi wa kikaokazi cha utambulisho wa mfumo wa Majis ulioboreshwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira,Dodoma.

About the author

mzalendoeditor