Featured Kitaifa

TUMEJIPANGA VYEMA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA – MCHENGERWA

Written by mzalendo

Na OR-TAMISEMI, Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) amesema ofisi yake imejipanga vyema Kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, kwa kushirikiana na Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo tarehe 16 Aprili, 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadilio ya Bajeti na mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024/25

Aidha amezitaka mamlaka za Mikoa na Halmashauri kuendelea Kusimamia shughuli za utawala bora, kukuza demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi na Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma (Diecentralization by Devolution – D by D).

Pia,Mhe. Mchengerwa amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea Kuratibu na kusimamia mkakati wa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi yasiyo na tija katika ngazi zote ikijumuisha kuongeza kasi ya biashara ya kaboni.

“Serikali kwa kushirikiana na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) inatarajia kutekeleza na kusimamia ajira, maadili na maendeleo ya walimu kwa kuhakikisha walimu wanasajiliwa, wanathibitishwa kazini na kwa wale wenye sifa wanapandishwa vyeo/wanabadilishiwa vyeo kwa wakati, pamoja na kusimamia maadili na nidhamu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari katika Utumishi wa Umma na kuwezesha mazingira bora ya kufanyia kazi.” Alisema Mhe. Mchengerwa

About the author

mzalendo