Featured Kitaifa

TBA DODOMA YAENDELEA KUTEKELEZA ZOEZI LA KUWAONDOA WADAIWA SUGU

Written by mzalendoeditor

Meneja wa Wakala wa Majengo TBA Mkoa wa Dodoma Bw.Emmanuel Wambura,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu katika eneo la Mwangaza Kisasa jijini Dodoma.

…………….

WAKALA wa Majengo nchini TBA Mkoa wa Dodoma umeendelea na zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu wa pango kwenye nyumba zao wakiwamo watumishi wa umma ambao taasisi zao zimeshindwa kulipa kodi huku wakibainisha kuwa zoezi hilo ni endelevu na litawafikia wadaiwa wote.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Aprili 16,2024 jijini Dodoma Meneja wa Wakala wa Majengo TBA Mkoa wa Dodoma Bw.Emmanuel Wambura amesema imekuwa ni tabia ya watumishi wa umma kukaa kwenye nyumba hizo bila kuzilipia kwa makusudi.

Wambura amesema kuwa kwasasa zipo hadi taasisi zimekaa mika 10 hazijalipa kodi hizo na kusema kluwa wataanza nazo.

“Kwahiyo tunategemea kuanza na taasisi zile ambazo zinadaiwa kuanzia miezi Mitatu na katika zoezi hili najua wengi watao kwenda kuguzwa zaidi ni viongozi ambao ni wataasisi hizi za umma kwasababu nao hawa ni wapangaji wetu sasa katika hili tunajua zipo changamoto mbalimbali zinaweza kujitpokeza hivyo tumeshazifanyia kazi kwani hawa ni viongozi wetu lazima tutumie hekima kukusanya kodi hizi,”amesema Wambura 

Wambura amesema taratibu zote wameshazifanya ikiwemo kuonana nao kwanza kiofisi pamoja na Wizara kuiandikia baada ya wao kuwa wameshawaandikia ujumbe hivyo wanaamini hiyo itakwenda kuondoa misuguano kati ya wao na hizo taasisi na watumishi huku vyombo vya ulizni na usalama navyo vikiwa vimeshirikishwa.

“Ukweli ni kwamba kutokukusanya kodi kutoka kwa watu hawa wakala unashindwa kujiendesha na kufanya tuendelee kutegemea Ruzuku kutoka Serikali kuu lakini pia nyumba za watumishi ni chache hapa Dodoma kiasi kwamba tunashindwa kuendelea kujenga nyingine kwasababu hatukusanyi tunategemea makusanyo haya yaende yakaendeleze pia katika milki ya serikali ili ijenge nyumba zaidi na watu wakapate nyumba,”amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twins Auction Mart, inayotekeleza oparesheni hiyo Bw. Zuber Hassan Lumbiza amesema kwasasa wanadili na taasisi kwani mwaka jana mwezi wa 12  walidili na watu wengine binafsi ambao walikuwa wanadaiwa hivyo leo wamekuja mahususi kwa taasisi hizo kwani hizo nyumba ni kwaajili yao.

“Uzuri wake kila mtu anajua wajibu wake na hii kodi ni kodi ya Serikali na kila mtu anahitajika alipe kwahiyo kuna changamoto katika kuwatao lakini hatuna jinsi na tumejipanga na tunaendelea kujipanga ilimradi tu pesa zilipwe na kama mtu atalipa tutamuacha aendelee kukaa lakini asipolipa tutamuondoa,”amesema.

Amesema taasisi alizokabidhiwa zinadaiwa ni 58 ambapo zinadaiwa takribani Shilingi Bilioni 1.1 huku tasisi 12 pekee ndizo zimekwisha kulipie deni hilo huku wakiwa wamekusanya Milioni 160 pekee huku utaratibu mwingine ukiwa unaendelea.

Meneja wa Wakala wa Majengo TBA Mkoa wa Dodoma Bw.Emmanuel Wambura,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu katika eneo la Mwangaza Kisasa jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji Twins Action Mart Dalali aliyepewa kazi ya kuwaondoa wadaiwa Sugu Bw.Emmanuel Wambura,akielezea hatua pamoja na zoezi lililofikia katika kuwaondoa wadaiwa Sugu Mkoa wa Dodoma.

Muonekano wa Vitu vikitolewa ndani wakati wa zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu katika nyumba za TBA Mkoa wa Dodoma.

About the author

mzalendoeditor